Kidato cha 3 & 4
Vitabu vinavyoichambua jamii na matatizo yake.
Vitabu : Watoto wa Maman’tilie na Joka la Mdimu
Mpitiaji: Mwl. Farid
KATIKA uhakiki huu tutaangalia namna vitabu hivi viwili: Watoto wa Maman’tilie na Joka la Mdimu vinavyofanana na kutofautiana.
Ipo tofauti baina ya vitabu hivi viwili, tofauti hiyo inajitokeza katika mambo mbalimbali yakiwemo haya:
Dhamira kuu.
Dhamira Kuu inayojitokeza katika Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie ni kuzungumzia juu ya watoto wa mitaani na hatima yao. Riwaya inaonesha namna watoto wanavyo poteza mwelekeo wa maisha pindi waachapo kusoma.
Zita Peter Musa Kurwa na Doto wametumiwa na mwandishi kuonyesha ukweli wa jambo hilo. Watoto hao baada ya kushindwa kuendelea na shule waliingia mitaani na hatimaye kujihusisha na vitendo viovu vikiwemo uuzaji wa dawa za kulevya na wizi.
Riwaya ya Joka la Mdimu kwa upande inazungumzia kuhusu ufisadi. Mwandishi kwa kutumia mbinu za Kifasihi anaelezea kuhusu wizi wa fedha za kigeni uliofanyika katika benki kuu na hivyo kusababisha serikali kukosa fedha za kununulia mafuta kutoka nje hali iliyosababisha nchi kukumbwa na hali ngumu kiuchumi.
“Hebu angalia hili tatizo la mafuta. Nasikia meli imekuja na mafuta, benki hakuna hata senti ya fedha za kigeni. Imegeuza na kurudi na kutuachia madeni ya kusafirisha mafuta hayo pamoja na ushuru wa bandari. Sasa kama usemavyo sukari inapelekwa nje, mbona tunashindwa kulipia mafuta.
Siasa na uongozi wa nchi
Dhamira nyingine inayoonyesha kutofutiana kwa vitabu hivi
ni dhana ya siasa na uongozi wananchi.
Watoto wa Maman’tilie haizungumzi jambo lolote kuhusu wanasiasa wetu, badala yake inaelekeza mjadala wake kwenye dhana ya uongozi wa kifamilia
Kuhusiana na suala zima la uongozi wa familia, riwaya hii imeonyesha namna wazazi wanavyotakiwa kuwa viongozi wazuri wa familia kwa kuwapa watoto malezi yanayowafanya kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yao wao wenyewe hapo baadaye.
Jambo hili tunaweza kuliona kupitia malezi ambayo mamantilie anawapa watoto wake.Mama huyo anawashirikisha Zita na Peter kwenye shughuli yake ya kupika na kuuza chakula. Na tunawaona Zita na Peter wakiyamdu maisha pale wanapobaki peke yao wakati Maman’tilie anaposafiri kwenda Matombo, Morogoro.
Riwaya ya Joka la Mdimu tofauti na Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie yenyewe imezungumzia kuhusu uongozi wa kitaifa.
Mwandishi anaelezea namna uongozi wa nchi ulivyo kiini cha matatizo ya kimaisha yanayowakabili wananchi walio wengi
Nafasi ya mwanamke katika jamii.
Tofauti kati ya Watoto wa Maman’tilie na Joka la Mdimu imejitokeza pia katika kipengele cha nafasi ya mwanamke.
Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie kwa kiasi kikubwa inamwonyesha mwanamke kama mzalishaji mali
Nafasi hiyo inajibainisha kupitia mhusika Maman’tilie kutokana na namna alivyokuwa akijishughulisha na kazi ya kupika na kuuza chakula.
Nafasi kama hiyo kwa kweli hatuioni katika Joka la Mdimu kwa kiwango kinachoweza kulinganishwa na hicho kionekanacho katika Watoto wa Maman’tilie.
Joka la Mdimu kwa upande wake inamwonesha mwanamke kama chombo cha starehe. Nafasi hii inajibainisha kutokana na namna Brown kwacha alivyokuwa akiwatumia wanawake mbalimbali kujistarehesha.
Athari za maendeleo ya sayansi na tekinolojia
Watoto wa Maman’tilie imeonyesha namna uvumbuzi wa video
ulivyoharibu vijana wetu. Vijana wetu kutokana na kuangalia picha za video zikiwemo zile zinazohusu ujambazi hatimaye nao pia huiga ujambazi huo na kutenda.
Riwaya hii inathibitisha ukweli huo kutokana na namna inavyoelezea kuhusu jinsi Dan na wenzake walivyopanga kwenda kuiba kwa Rhemtulah kwa kutumia mbinu za ujambazi ambazo walikuwa wakiziona katika picha za video.
Lazima mambo yaende kimafia Dan alikuwa kaathirika sana na
Video za ujambazi wa ulaya (uk.41)
Dhamira kama hii hatuioni katika Joka la mdimu
Tatizo la imani za ushirikina
Dhamira hii amejitokeza katika Joka la Mdimu. Mtunzi anatueleza namna imani za ushirikina zilivyoenea katika jamii
Kiasi cha kutumiwa hata katika shughuli za michezo.
Jambo hilo linaonyeshwa na mtunzi pale anapoelezea kuhusu mechi kati ya timu mbili tofauti za mpira; timu ya City Devils na Sega Warriors (uk. 58-59) Dhamira hii haikujitokeza katika Watoto wa Mamantilie.
Tofauti kati ya Joka la Mdimu na Watoto wa Maman’tilie inajitokeza na katika fani pia; katika vipengele tofauti vikiwemo hivi:
Wahusika:
Joka la Mdimu inatumia wahusika wa kawaida na wahusika vielelezo. Hawa ni wahusika ambao hupewa majina kulingana
na aidha tabia zao au umbile lao, kazi zao n.k.
Wahusika hao ni Brown kwacha na Dakta Mikwala. Brown Kwacha ni mtu apendaye pesa na Dakta Mikwala pia ni mtu apendaye rushwa ingawaje mwanzoni huwapiga mkwara watu ili kutaka kuonyesha kuwa yeye si mla rushwa
Mandhari.
Joka la Mdimu mandhari yake haitajwi wazi, Watoto wa Maman’tilie Madhari yake imetajwa wazi kuwa ni Dar es salam na vitongozi vyake: ambavyo ni Kisutu, Manzese na Tabata.
Jina la kitabu
Tofauti kati ya vitabu hivi imejitokeza pia kwenye kiini cha majina. Jina la Joka la Mdimu limetokana na dhana ya Uongozi. Mwandishi anawalinganisha viongozi wasiofaa na nyoka wa kijani aishiye katika mdimu ambapo unaweza ukadhani ni mdimu kumbe ni nyoka.
Na viongozi pia baadhi yao kwa mtazamo wa kawaida huonekana kama wapo upande wa wananchi kumbe ni wasaliti.
Jina la Watoto wa Maman’tilie limetokana na mhusika mkuu Maman’tilie.

No comments:
Post a Comment