Kuainisha sentensi kulingana na uamilifu wake kimawsiliano
- Sentensi za taarifa, mfano. Mwalimu ameondoka darasani
- Sentensi ulizi, Mfano; Mwalimu amekwenda wapi?
- Sentensi agizi, Niletee hilo daftari!
- Sentensi ya masharti, Ungewahi nisinge kupa adhabu.
- Sentensi za kukanusha, Mimi sikumpiga Beti
Aina za sentensi kimuundo
Sentensi sahili: Ni sentensi ambayo huundwa na kishazi huru kimoja. Sentensi ya aina hii huwa inaelezea taarifa moja tu. Mfano; Wanafuzi wanafanya mtihani; Walinzi walitaka kunizuia nisiingiendani.
Miundo ya sentensi sahili
- Muundo wa kitenzi kikuu peke yake. Mfano: Gari limeanguka
- Muundo wa kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi. Mfano: Mgosiyuda alitaka (TS) nisipate (T) utajiri
- Muundo wa vira-vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi ‘kuwa’. Mfano: John amekuwa akiangalia TV kwa muda mrefu sana.
- Muundo wa kitenzi shirikishi. Mfano: Kiswahili ni tunu ya Taifa.
Sifa za sentensi sahili
- Ina kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeachwa kutajwa kwa kuwa kinaeleweka.
- Ina kiarifu ambacho kimeundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi au kitenzi kishirikishi na kijalizo na chagizo.
- Haifungamani na sentensi nyingine na hivi inajitosheleza kimuundo na kimaana.
Sentensi changamano: Hii ni sentensi yenye kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi. Sifa moja kubwa ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi ambacho hutegemea kishazi kingine huru ndani ya sentensi hiyo. Msingi muhimu wa uhusiano ndani ya sentensi hizo ni ule wa kishazi kimoja kutegemea kingine.
Miundo ya sentensi changamano
- Muundo yenye vishazi virejeshi. Mfano: Gari liliopinduka jana jioni halikuharibika hatata kidogo.
Sentensi ambatano: Hii ni sentensi inayojengwa na sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia viunganishi kama vile likini, wala, au, na, nakadhalika.
Miundo ya sentensi ambatano
- Miundo yenye sentensi sahili tu. Mfano: Mwalimu anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele.
- Miundo yenye sentensi sahili na changamano. Mfano: Walinzi waliposhindwa polisi waliwasaidia lakini hawakuweza kuwakamata majambazi.
- Miundo yenye sentensi changamano tu. Mfano: Barabara zilizojengwa na wakoloni zimedumu hadi leo wakati zile zilizojengwa na Wachina hata mwezi hazifikishi.
- Miundo yenye vishazi visivyounganishwa kwa viunganishi.
No comments:
Post a Comment