Ufahamu
Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.
Aina za ufahamu
Kuana aina kuu mbili za ufahamu ambazo ni ufahamu wa kusoma na uafahamu wa kusikiliza.
a. Ufahamu wa kusoma
Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu cha habari, kitabu au gazeti.
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatkiwa ajiluze, Je, kinachoongelewa hapa nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.
- Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
- Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.
- Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzurijuu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.
b. Ufahamu wa kusikiliza
Ufahamu wa kusikiliza ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusikiliza habari fulani, anaweza kusikiliza kwa kusimuliwa, kusomewa au kupitia redio na rekodi.
Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:
- Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.
- Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
- Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadae.
- Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.
Kufupisha habari
Kufupisha habari ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache lakini bila kupotosha ujumbe wa habari ya kwanza.
Ufupisho wa habari huwa na sifa hizi:
- Huwa ni mfupi kuliko habari ya mwanzo
- Huwa na ujumbe uleule uliokuwa katika habari ya mwanzo
- Hujumuisha mawazo makuu yaliyodondolewa kutoka kwenye habari ya mwanzo
- Mawazo haya sharti yapangwe katika mtririko wenye mantiki
Hatua za kufuata katika kuandika ufupisho
Ili kuweza kufanikiwa kufupisha habari kwa ufanisi hatua zifuatzo sharti zifuatwe:
- Kuisoma au kuisilikiza habari kwa makini ili kuielewa vizuri
- Kutambua na kubaini mawazo makuu yanayojitokeza katika kila aya
- Kuyaunganisha mawazo makuu na kuandika au kuelezea ufupisho wa habari hiyo kwa maneno yako mwenyewe bila kupostosha maana ya habari ya kwanza.
- Kuhesabu idadi ya maneno ya ufupisho ili kuyapunguza ikiwa yanazidi idadi iliyotakiwa.
- Kama muda unaruhusu pitia tena habari ya mwanzo na pitia tena ufupisho ili kujiridhisha kuwa hujaacha taarifa yoyote ya muhimu.
Hongera kwa kazi nzuri
ReplyDeleteNimeipenda.
safi sana kwa elimu bola
ReplyDeleteEnter your comment...hongera na ahsante
ReplyDeleteAsante
ReplyDelete