Ahlus-Sunnah
wal-Jamaa’ah wanaamini kwamba baadhi ya Waislamu wataingia Peponi bila
ya kufanyiwa hesabu au kupewa adhabu. Wengine wataingia Peponi baada ya
kufanyiwa hesabu, Wengine wataingia Peponi baada ya kuadhibiwa motoni
kama Anavyotaka Allaah kisha Atawatoa humo.
Kutolewa
motoni kisha kuingizwa Peponi hakutawasababishia huzuni au dhiki Peponi
kwasababu Pepo ni makazi ya raha tupu. Kama ilivyotajwa katika Qur-aan
na Sunnah, watapata kila walichokipata wakaazi wengine wa Peponi.
Hakuna
dalili inayoashiria kwamba watu hao watakuwa na hisia za majuto baada
ya kuingia kwao Peponi kutokana na adhabu watakazozipata motoni.
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametutajia hali zao zitakavyokuwa baada ya kutolewa motoni kama ifutavyo:
1. Watatumbukizwa Kwenye Mto Wa Uhai Wabadilike Kuwa Wapya
Imesimuliwa
kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((إِذَا دَخَلَ أَهْلُ الْجَنَّةِ الْجَنَّةَ وَأَهْلُ النَّارِ النَّارَ يَقُولُ اللَّهُ : مَنْ كَانَ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالُ حَبَّةٍ مِنْ خَرْدَلٍ مِنْ إِيمَانٍ فَأَخْرِجُوهُ، فَيَخْرُجُونَ، قَدْ امْتُحِشُوا، وَعَادُوا حُمَمًا، فَيُلْقَوْنَ فِي نَهَرِ الْحَيَاةِ ، فَيَنْبُتُونَ
كَمَا تَنْبُتُ الْحِبَّةُ فِي حَمِيلِ السَّيْلِ)) وَقَالَ النَّبِيُّ
صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَلَمْ تَرَوْا أَنَّهَا تَنْبُتُ صَفْرَاءَ مُلْتَوِيَةً)) رواه البخاري ومسلم
((Watu
wa Peponi watakapoingia Peponi watapaoingia Peponi na wa motoni
watakapoingia motoni, Allaah Atasema [kuwaambia Malaika]: “Yeyote
aliyekuwa na Iymaan moyoni mwake, uzito wa chembe cha atomu, mtoeni!”
Watamtoa humo, watatoka kama kwamba ni mifupa iliyounguzwa na
watabadilika kuwa makaa. Watatumbukizwa katika mto wa uhai, kisha
watakuwa [kimaumbile] humo kama mfano wa mbegu zinapomea katika ufa
[mwatuko] wa mafuriko)). Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi
wa sallam): ((Je huwaoni wanavyomea [wanavyokuwa kimaumbile] manjano na
kupinda?)). [Al-Bukhaariy na Muslim].
2. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba watabadilika watakapotolewa motoni.
Imesimuliwa
toka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusu Jahannamiyuwn (watu wa
motoni):
((يَخْرُجُونَ مِنْ النَّارِ بَعْدَ أَنْ يَكُونُوا فِيهَا، فَيَخْرُجُونَ كَأَنَّهُمْ عِيدَانُ السَّمَاسِمِ، فَيَدْخُلُونَ نَهَرًا مِنْ أَنْهَارِ الْجَنَّةِ فَيَغْتَسِلُونَ فِيهِ فَيَخْرُجُونَ كَأَنَّهُمْ الْقَرَاطِيسُ)) رواه مسلم
((Watatolewa motoni baada ya kuweko humo. Kisha watatoka kama
kwamba ni matawi ya chembe za ufuta. Kisha wataingia katika Mto
miongoni mwa mito ya Peponi ambako wataoga kisha watatoka [weupe] humo
kama karatasi)). [Muslim].
Imaam An-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema: “Ufuta imekusudiwa chembe za ufuta maarufu zinazotoa mafuta ya ufuta”.
Imaam
Abu as-Sa’adaat al-Mubaarak bin Muhammad bin ‘Abdil-Kariym al-Jazariyy
anayejulikana kama: Ibn Al-Athiyr (Rahimahu Allaah) amesema:
“Inamaanisha - na Allaah Anajua zaidi – kwamba matawi ya ufuta
yanapokusanywa na kuachwa juani ili mbegu zake zikusanywe, hubadilika
kuwa membamba na meusi kama kwamba zimeunguzwa. Ndio wakafananishwa watu
hawa. Kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). ((Kisha watatoka humo kama karatasi))
wamefananishwa kama karatasi kwa sababu watakuwa weupe mno baada ya
kuoga mtoni na weusi wote waliokuwa nao utaondoshwa.” [Sharh Muslim].
Kadhaalika, imesimuliwa na Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((يَخْرُجُ مِنْ النَّارِ بِالشَّفَاعَةِ كَأَنَّهُمْ الثَّعَارِيرُ، قُلْتُ: مَا الثَّعَارِيرُ؟ قَالَ: الضَّغَابِيسُ)) البخاري
((Watatoka motoni kwa sababu ya shafa’ah (uombezi) wakiwa kama matango)). [Al-Bukhaariy].
Al-Haafidhw
Ibn Hajr al-‘Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema: “Kuhusu matango
madogo, makusudio ni, kama kitu cheupe na kidogo”
Tanbihi:
Sifa
ya weupe huu unakusudiwa vile watakavyokuwa baada ya kukua (kumea)
[Fat-h al-Baaariy (11/429)]. Lakini mwanzo watakapotoka motoni watakuwa
kama makaa kama inavyoelezea Hadiyth ifuatayo:
3. Watakua kama Lulu kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atawaruzuku Radhi Zakke na Hatawaghadhibikia tena.
Imesimuliwa
kutoka kwa Abu Sa’iyd al-Khudriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((فَيَقُولُ
اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ : شَفَعَتْ الْمَلَائِكَةُ، وَشَفَعَ
النَّبِيُّونَ، وَشَفَعَ الْمُؤْمِنُونَ، وَلَمْ يَبْقَ إِلَّا أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ، فَيَقْبِضُ قَبْضَةً مِنْ النَّارِ فَيُخْرِجُ مِنْهَا قَوْمًا لَمْ يَعْمَلُوا خَيْرًا قَطُّ قَدْ عَادُوا حُمَمًا، فَيُلْقِيهِمْ فِي نَهَرٍ فِي أَفْوَاهِ الْجَنَّةِ يُقَالُ لَهُ " نَهَرُ الْحَيَاةِ " فَيَخْرُجُونَ كَمَا تَخْرُجُ الْحِبَّةُ فِي حَمِيلِ السَّيْلِ ... قَالَ : فَيَخْرُجُونَ كَاللُّؤْلُؤِ فِي رِقَابِهِمْ الْخَوَاتِمُ ، يَعْرِفُهُمْ أَهْلُ الْجَنَّةِ، هَؤُلَاءِ عُتَقَاءُ اللَّهِ الَّذِينَ أَدْخَلَهُمْ اللَّهُ الْجَنَّةَ بِغَيْرِ عَمَلٍ عَمِلُوهُ وَلَا خَيْرٍ قَدَّمُوهُ ، ثُمَّ يَقُولُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ فَمَا رَأَيْتُمُوهُ فَهُوَ لَكُمْ، فَيَقُولُونَ : رَبَّنَا أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ الْعَالَمِينَ، فَيَقُولُ لَكُمْ عِنْدِي أَفْضَلُ مِنْ هَذَا ، فَيَقُولُونَ: يَا رَبَّنَا أَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ هَذَا، فَيَقُولُ رِضَايَ فَلَا أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا)) رواه البخاري ومسلم
((Allaah
Atasema [Peponi]: “Malaika wameshaombea shafa’ah, Mitume wameshaombea
shafa’ah, Waumini wameshaombea shafa’ah, hakuna aliyebakia isipokuwa
Mwingi wa Rahma, Mwenye Kurehemu kuliko wote wanaorehemu.” Kisha Atateka
kutoka motoni na Atatoa watu wasiopata kufanya jema lolote [duniani] na
ambao wamebadilika kuwa makaa. Atawatumbukiza katika Mto ulio kingoni
kwa Peponi unaoitwa ‘Mto wa Uhai’ watatoka humo kama zinavyotoka mbegu
katika ufa wa mafuriko. Kisha watatoka wakiwa kama lulu wakiwa na
mapambo shingoni mwao na watu wa Peponi watawatambua. Hawa ni
waliofidiwa [waliokombelewa] na Allaah Akawaingiza Peponi bila hata ya
kuwa wametenda ‘amali njema au kheri yoyote waliyoitanguliza. Kisha
Atasema: “Ingieni Peponi, mtakayoyaona humo ni yenu.” Watasema: “Ee Mola
wetu, Umetupa ambayo Hujapatapo kumpa yeyote kati wa walimwengu.”
Atasema: “Mtapata kutoka Kwangu yaliyo bora kuliko haya” Watasema: “Ee
Mola wetu! Kitu gani tena kitakachokuwa bora kuliko haya?” Atasema:
“Radhi Zangu kwani Sitoghadhibika tena nanyi kamwe.”)) [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hii
ni Hadiyth muhimu ambayo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) ametaja daraja ya juu kabisa itakavyokuwa ya watu watakaotolewa
motoni ambao Mola wao Atawaruzuku, karama, heshima, na fadhila zikiwemo:
· Kutumbukizwa katika Mto wa Uhai ili wakuwe (waumbike) kama wapya.
· Kutoka katika Mto kama kwamba lulu wakiwa wamevaa mapambo shingoni mwao.
· Kupewa kila watakachokiona Peponi.
· Kudhania
kwao kutokana na kheri na baraka na furaha ya hali ya juu watakayoipa
kwamba Allaah Amewakirimu kwa jambo Hajapatapo kumkirimu yeyote
mwengine.
· Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atawaruzuku Radhi Zake na Hatowaghadhibikia tena kamwe.
Daraja ambazo Allaah Atawakirimu watu watakoingia Peponi zimethibitika katika usimulizi ufuatao wa Hadiyth:
Imesimuliwa
kutoka kwa ‘Abdulllaah bin Mas’uwd (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((إِنِّي لَأَعْلَمُ آخِرَ أَهْلِ النَّارِ خُرُوجًا مِنْهَا وَآخِرَ أَهْلِ الْجَنَّةِ دُخُولًا، رَجُلٌ يَخْرُجُ مِنْ النَّارِ كَبْوًا فَيَقُولُ اللَّهُ: اذْهَبْ فَادْخُلْ الْجَنَّةَ، فَيَأْتِيهَا فَيُخَيَّلُ إِلَيْهِ أَنَّهَا مَلْأَى، فَيَرْجِعُ فَيَقُولُ: يَا رَبِّ وَجَدْتُهَا مَلْأَى، فَيَقُولُ: اذْهَبْ فَادْخُلْ الْجَنَّةَ، فَيَأْتِيهَا فَيُخَيَّلُ إِلَيْهِ أَنَّهَا مَلْأَى، فَيَرْجِعُ فَيَقُولُ: يَا رَبِّ وَجَدْتُهَا مَلْأَى، فَيَقُولُ: اذْهَبْ فَادْخُلْ الْجَنَّةَ، فَإِنَّ لَكَ مِثْلَ الدُّنْيَا وَعَشَرَةَ أَمْثَالِهَا)) - أَوْ: ((إِنَّ لَكَ مِثْلَ عَشَرَةِ أَمْثَالِ الدُّنْيَا - فَيَقُولُ: تَسْخَرُ مِنِّي)) - أَوْ: ((تَضْحَكُ مِنِّي - وَأَنْتَ الْمَلِكُ)) فَلَقَدْ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ضَحِكَ حَتَّى بَدَتْ نَوَاجِذُهُ، وَكَانَ يَقُولُ: ((ذَاكَ أَدْنَى أَهْلِ الْجَنَّةِ مَنْزِلَةً)) رواه البخاري ومسلم
((Nawajua
watu wa mwisho kabisa watakaotoka motoni, na watu wa mwisho kabisa
watakaoingia Peponi. Atakuwa ni mtu atakayetoka akitambaa kutoka motoni
kisha Allaah Atamwambia: “Nenda na ungie Peponi” Ataifikia lakini
atadhania kwamba imejaa. Atarudi na kusema: “Mola wangu! Nimeikuta
imejaa!” Allaah Atasema: “Nenda ingia Peponi” Atafikia lakini atadhania
kwamba imejaa. Atarudi na kusema: “Mola wangu! Nimeikuta imejaa!” Allaah
Atasema: “Nenda ingia Peponi, kwani utapata mfano wa dunia na mara kumi
yake”)) Au: ((“Utapata mfano wa mara kumi ya dunia” Atasema [mja]: “Je
unanifanyia masikhara?)) Au: ((“Je unanidhihaki na hali Wewe ni
al-Malik?”)). Nikamuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) akicheka mpaka magego yake yakadhihirika na huku
akisema: ((Huyo ndiyo mtu wa daraja ya chini kabisa Peponi)). [Al-Bukhaariy na Muslim].
4. Watajulikana
kama ni Al-Jahannamiyuwn (watu wa motoni) au ‘Utaqaa al-Jabbaar’
(waliokombolewa na Mwenye Ujabari) Kisha wataondoshewa jina hilo.
Jina la Al-Jahannamiyuwn ni wingi wa Jahannam yaani moto. Ina maana kwamba Allaah Amewakomboa motoni.
Imesimuliwa
kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((يَخْرُجُ قَوْمٌ مِنْ النَّارِ بَعْدَ مَا مَسَّهُمْ مِنْهَا سَفْعٌ فَيَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ فَيُسَمِّيهِمْ أَهْلُ الْجَنَّةِ الْجَهَنَّمِيِّينَ)) رواه البخاري
((Miongoni
mwa watu watatolewa motoni baada ya miale yake imewagusa [na
kuwabadilisha rangi] kisha wataingizwa Peponi. Na watu wa Peponi wataiwa
al-Jahannamiyuwn)). [Al-Bukhaariy].
Na pia kauli nyingine kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu): kwa Hadiyth iliyokusanywa na Imaam Ahmad:
((... فَيَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ فَيَقُولُ لَهُمْ أَهْلُ الْجَنَّةِ: هَؤُلَاءِ الْجَهَنَّمِيُّونَ! فَيَقُولُ الْجَبَّارُ: بَلْ هَؤُلَاءِ عُتَقَاءُ الْجَبَّارِ عَزَّ وَجَلَّ))
((…wataingia
Peponi na watu wa Peponi watasema: “Hawa ni Al-Jahannamiyuwn lakini
Al-Jabbaar [Mwenye Ujabari] Atasema: “Hapana! Bali wao ni waliokombolewa
na Al-Jabbaar ‘Azza wa Jalla)). [Imepewa
daraja ya Swahiyh na Ibn Mandah katika ‘al-Iymaan’ (2/847), Ibn
Khuzaymah (2/710) na Al-Albaaniy katika ‘Hukm Taarik As-Swalaah’ (uk.
33).
Ibn Hibbaan amesimulia kutoka kwa Abu Sa’iyd al-Khudriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu):
((فَيُسَمَّوْنَ فِي الْجَنَّةِ الْجَهَنَّمِيِّينَ مِنْ أَجْلِ سَوَادٍ فِي وُجُوهِهِمْ، فَيَقُولُونَ : بَّنَا أَذْهِبْ عَنَّا هَذَا الاسْمَ ، قَالَ : فَيَأْمُرُهُمْ فَيَغْتَسِلُونَ فِي نَهْرِ الْجَنَّةِ , فَيَذْهَبُ ذَلِكَ مِنْهُمْ)).
((Wataitwa
humo Peponi: “al-Jahannamiyyuwn” kutokana na weusi katika nyuso zao.
Watasema: “Mola wetu! Tuondoshee jina hili!”)) Akasema: ((Kisha
Atawaamrisha waoge katika Mto wa Peponi, wataondoshewa hilo [Jina])). [Imepewa daraja ya Swahiyh na Ibn Hibbaan (16/457) na pia Ash-Shu’ayb al-‘Arnauwtw].
Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia kwamba mchovyo
mmoja tu wa Peponi utamfanya Muislamu asahau tabu zote alizozokabiliana
nazo duniani, itakuwaje basi ikiwa Pepo ndio makazi yake ya milele?
Imesimuliwa
kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((يُؤْتَى بِأَنْعَمِ أَهْلِ الدُّنْيَا مِنْ أَهْلِ النَّارِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيُصْبَغُ فِي النَّارِ صَبْغَةً ثُمَّ يُقَالُ : يَا ابْنَ آدَمَ هَلْ رَأَيْتَ خَيْرًا قَطُّ ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ نَعِيمٌ قَطُّ ؟ فَيَقُولُ : لَا وَاللَّهِ يَا رَبِّ ، وَيُؤْتَى بِأَشَدِّ النَّاسِ بُؤْسًا فِي الدُّنْيَا مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيُصْبَغُ صَبْغَةً فِي الْجَنَّةِ فَيُقَالُ لَهُ : يَا ابْنَ آدَمَ هَلْ رَأَيْتَ بُؤْسًا قَطُّ ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ شِدَّةٌ قَطُّ ؟ فَيَقُولُ : لَا وَاللَّهِ يَا رَبِّ مَا مَرَّ بِي بُؤْسٌ قَطُّ، وَلَا رَأَيْتُ شِدَّةً قَطُّ)) رواه مسلم
((Mtu
aliyeneemeka kabisa duniani ambaye ni miongoni mwa watu wa motoni
ataletwa Siku ya Qiyaamah na atachovywa mara moja motoni kisha
ataulizwa: “ee mwanadamu! Umepatapo kuona zuri lolote? Umewahi
kupata raha yoyote?” Atasema: “Hapana Mola wangu!” Kisha ataletwa mtu
aliyepata shida kabisa duniani akiwa miongoni mwa wa watu wa Peponi
atachovywa Peponi ataambiwa: “Ee mwanadamu! Je umepatapo kuona ubaya
wowote? Je imekupitia shida yoyote?” Atasema: “Hapana Mola wangu!
Sijapatapo kuona ubaya wowote wala haijanipitia shida yoyote.”)) [Muslim].
Dalili
nyingine kwamba mchovyo mmoja wa neema za Pepo utamuondoshea tabu zote
za awali, mpaka tabu za kuadhibiwa motoni. Hivi ni kuhusiana na
yaliyotajwa kuhusu kubadilishwa kwake mtu baada ya kutumbukizwa katika
‘Mto wa Uhai’ ni katika mapokezi yaliyosimuliwa na Imaam Muslim (2836)
kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaah ‘anh) kutoka kwa Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amesema:
((مَنْ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ يَنْعَمُ لَا يَبْأَسُ لَا تَبْلَى ثِيَابُهُ وَلَا يَفْنَى شَبَابُهُ))
((Atakayeingia Peponi atastarehe na hatokuwa na kuhuzunika, nguzo zake hazitochakaa wala ujana wake hautatoweka [hatozeeka])).
Neema
hiyo inathibitisha kwamba atakayeingizwa Peponi ataondoshewa tabu zote
na inamaanisha kwa ujumla kila atakayeingia Peponi, ikiwa ni mwenye
kuingizwa motoni kwanza au hakuingizwa.
Al-Qaadhwiy
amesema: “Kinachomaanishwa hapa ni kwamba Pepo ni makazi ya kuthibiti
na neema ambazo hazitobadilika au kuathirika kwa tabu zozote au
ufisadi.” [Tuhfat al-Ahwadhi (7/194)].
Kwa sababu hizo, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatuambia hali za watu wa Peponi watakapoingia:
((وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَذْهَبَ عَنَّا الْحَزَنَ إِنَّ رَبَّنَا لَغَفُورٌ شَكُورٌ* الَّذِي أَحَلَّنَا دَارَ الْمُقَامَةِ مِنْ فَضْلِهِ لا يَمَسُّنَا فِيهَا نَصَبٌ وَلا يَمَسُّنَا فِيهَا لُغُوبٌ))
((Na
watasema: “AlhamduliLLah – Himdi Zote ni za Allaah [Pekee] Ambaye
Ametuondoshea huzuni [zote]. Hakika Mola wetu bila shaka ni Mwingi wa
Kughufuria, Mwenye Kupokea Shukurani. Ambaye Ametuweka nyumba za makazi
kwa Fadhila Zake, haitugusi humo tabu wala haitugusi humo machovu)). [Faatwir: 34-35].
‘Allaamah
As-Sa’diy (Rahimahu Allaah) amesema: “Inamaanisha maskani ya makazi ya
milele, maskani ambayo mtu atataka kuishi milele kwa sababu ya mazuri
mengi yaliyomo humo na kwa sababu ya starehe zinazodumu na kwa sababu ya
kutokuweko cha kuondosha starehe hizo.
Na hayo ni kutokana ((kwa Fadhila Zake)) kwetu na Neema Zake, si kwa sababu ya ‘amali zetu, kwani ingelikuwa si Fadhila Zake, tusingelifikia tulivyofikia.
((haitugusi humo tabu wala haitugusi humo machovu)) yaani, hakutakuweko na machofu katika miili yetu, nyoyo au nguvu, wala katika raha nyingi. Hii
inaonyesha kwamba Allaah Atafanya miili yao iumbike vizuri upya na
Atawafanyia kila sababu za kuwafanyia makazi yao yawe ni yenye raha za
kudumu, ili wasiguswe na tabu au wahka wala huzuni.” [Tafsiyr As-’Sa’dy
689].
Na Allaah Anajua zaidi
No comments:
Post a Comment