HADIYTH ARUBAINI ZA IMAAM AN-NAWAWIY
Hadithi Ya 01: Kila Kitendo Kwa Nia Yake
الحديث الأول
" إنما الأعمال بالنيات "
عن أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى، فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا يُصِيبُها أو امْرأةٍ يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه)).
رَوَاهُ إِمَامَا الْمُحَدِّثِينَ أَبُو عَبْدِ اللهِ مُحَمَّدُ بنُ إِسْمَاعِيل بن إِبْرَاهِيم بن الْمُغِيرَة بن بَرْدِزبَه الْبُخَارِيُّ وَأَبُو الْحُسَيْنِ مُسْلِمٌ بنُ الْحَجَّاج بن مُسْلِم الْقُشَيْرِيُّ النَّيْسَابُورِيُّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا فِي "صَحِيحَيْهِمَا" اللذينِ هُمَا أَصَحُّ الْكُتُبِ الْمُصَنَّفَةِ.
HADITHI YA 1
KILA KITENDO KWA NIA YAKE
Kutoka kwa Amiri wa Waumuni, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattaab رضى الله عنه ambaye alisema : Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu صلى الله
عليه وسلم akisema:
Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokusudia. Kwa hivyo yule aliyehama kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, uhamaji wake ni kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, na yule ambae uhamaji wake ulikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (Fulani) uhamaji wake ulikuwa kwa kile kilichomuhamisha.
Imesimuliwa na Maimam wawili mabingwa wa hadithi Abu Abdalla Muhammad Ibn Ismail Ibn Ibrahim Ibn Mughiyra Ibn Bardizbah Al Bukhari na Abu Al Husayn Muslim Ibn Al-Hajjaj Ibn Muslim Al Qushayri An-Naysaburi, katika sahihi zao mbili ambavyo ni vitabu vya kutegemewa.
**********************
Hadithi Ya 02: Kuja Kwa Jibriyl عليه السلام Kuwafundisha Waislamu Mambo Ya Dini Yao
HADITHI YA 2
KUJA KWA JIBRIIL عليه السلام KUWAFUNDISHA WAISLAMU MAMBO YA DINI YAO
الحديث الثاني
"مجىء جبريل ليعلم المسلمين أمر دينهم"
عَن عُمَر رضي اللهُ عنه أَيْضاً قال: بَيْنَما نَحْنُ جُلْوسٌ عِنْدَ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ذات يَوْم إذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَياضِ الثِّيَاِبِ شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عليه أَثَرُ السَّفَرِ ولا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتى جَلَسَ إلى النَّبِّي صلى الله عليه وسلم، فأسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إلى رُكْبَتَيْهِ ووَضَعَ كَفَّيْهِ على فَخِذَيْهِ، وقال: يا محمَّدُ أَخْبرني عَن الإسلامِ، فقالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم:(( الإسلامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله، وتُقِيمَ الصَّلاةَ، وتُؤتيَ الزَّكاةَ، وتَصُومَ رَمَضان، وتَحُجَّ الْبَيْتَ إن اسْتَطَعتَ إليه سَبيلاً)). قالَ صَدَقْتَ. فَعَجِبْنا لهُ يَسْأَلُهُ ويُصَدِّقُهُ، قال : فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: ((أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ وشَرِّهِ)) قال صدقت. قال : فأخْبرني عَنِ الإحْسانِ. قال:(( أنْ تَعْبُدَ الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك)). قال: فأَخبرني عَنِ السَّاعةِ، قال: ((ما المَسْؤولُ عنها بأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ )). قال: فأخبرني عَنْ أَمَارَتِها، قال:(( أن تَلِدَ الأمَةُ رَبَّتَها، وأَنْ تَرَى الحُفاةَ العَُراةَ العالَةَ رِعاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ في الْبُنْيانِ )) ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيّاً، ثُمَّ قال : ((يا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟)) قُلْتُ: اللهُ ورسُولُهُ أَعلَمُ . قال:(( فإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 2
Kutoka kwa 'Umar رضى الله عنه ambaye amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume صلى الله عليه وسلم , hapo alitokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Mtumeصلى الله عليه وسلم akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Mtume) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ewe Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu. Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه وسلمalisema: Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mola isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mjumbe wake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.
(Akasema yule mtu yaani Jibriyl) Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake Mtume na kumsadikisha. Na akasema tena: Niambie kuhusu Iymaan. Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم) Ni kumwamini Mwenyeezi-Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake na siku ya Qiyaama, na kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake (Allaah سبحانه وتعالى ). (Akasema Jibriyl): Umesema kweli, akasema hebu nielezee kuhusu Ihsaan. Akasema Mtume صلى الله عليه وسلم Ni kumuabudu Allaah سبحانه وتعالى kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona. Akasema (Jibriyl): Niambie kuhusu Qiyaama. Akajibu (Mtume صلى الله عليه وسلم : Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji. Kisha akamwambia: Nijulishe alama zake: Akajibu (Mtume صلى الله عليه وسلم): Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya fahari. Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari). Kisha akasema Mtume صلى الله عليه وسلم : "Ewe 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Allaah na Mjumbe wake wanajua zaidi. Akasema Mtume صلى الله عليه وسلم: Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.
Hadithi Ya 03: Nguzo Za Kiislamu Ni Tano
الحديث الثالث
"بني الإسلام على خمس"
عن أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ: (( بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ : شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ )).
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 3
NGUZO ZA KIISLAMU NI TANO
Kutoka kwa Abu Abdur-Rahman Abdullah Ibn 'Umar Ibn Al-Khattaab رضي الله عنه Ambaye alisema: Nilimsikia Bwana Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: Uislamu umejengwa kwa nguzo tano:
Shahada kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mjumbe wake, kuswali, kutoa Zaka, kuhiji (Makka) na kufunga Ramadhan.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
**********************
Hadithi Ya 04: Hakika Umbo La Kila Mmoja Wenu Linakusanywa Katika Tumbo La Mama Yake
الحديث الرابع
"إن أحدكم يجمع في بطن أمه"
عن أبي عبْدِ الرَّحْمن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قال: حدَّثَنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وهُوَ الصَّادقُ المَصْدوق: (( إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يُرْسَلُ إليه المَلكُ فَيَنْفخُ فيه الرُّوحَ ويُؤمَرُ بأرْبَعِ كلماتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ وأَجَلِهِ وعَمَلِهِ وشَقيٌّ أو سَعيدٌ، فَوَاللهِ الَّذي لا إله غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ ليَعْمَلُ بعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ حتى ما يكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَليْه الكِتابُ فَيَعْمَلُ بعَملِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُها. وإنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهل النَّارِ حتى ما يَكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكتابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهل الجنَّةِ فَيَدْخُلُها))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 4
HAKIKA UMBO LA KILA MMOJA WENU LINAKUSANYWA KATIKA TUMBO LA MAMA YAKE.
Kutoka kwa Abu Abdur-Rahman Abdullaah Ibn Masu'ud رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم naye ndie mkweli, anaesadikiwa alitueleza haya:
Hakika umbo la kila mmoja wenu linakusanywa pamoja katika tumbo la mama yake kwa muda wa siku arubaini, ikiwa katika hali ya mbegu, baadaye tone la damu kwa muda kama huo, tena huwa ni kipande cha nyama kwa muda kama huo, tena hupelekwa Malaika anaempulizia pumzi za uhai na anaamrishwa mambo manne: kuandika rizki yake, maisha yake, amali yake na akiwa atakuwa (mtu) mbaya au mwema. Kwa Allaah ambaye hakuna Mungu isipokuwa Yeye, mmoja katika nyinyi hufanya vitendo vya watu wa peponi mpaka baina yake na pepo ikawa dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja katika nyinyi hufanya amali ya watu wa motoni mpaka baina yake na moto ikawa dhiraa, na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya amali ya watu wa peponi akaingia peponi.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim.
Hadithi Ya 05: Atakayezua Kitu Kisichokuwemo Katika Jambo Hili Letu Kitakataliwa
الحديث الخامس
" من أحدث في أمرنا هذا ما ليس منه فهو رد"
عن أُمِّ المُؤمِنينَ أُمِّ عَبْدِ الله عائِشَةَ رَضي اللهُ عنها قالَتْ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ أَحْدَثَ في أَمْرِنا هذا ما لَيْسَ منهُ فَهُوَ رَد))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ
((مَن عَمِلَ عَمَلاً لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ )).
HADITHI YA 5
ATAKAYEZUA KITU KISICHOKUWEMO KATIKA JAMBO HILI LETU KITAKATALIWA
Kutoka kwa Mama wa Waislamu Ummu Abdallah ‘Aisha رضى الله عنها ambaye alisema: Mtume wa Allaah سبحانه وتعالى kasema:
Yule anayezua kitu kisichokuwemo (kisichokuwa) katika jambo (DINI) hili letu kitakataliwa .
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim. Na katika usimulizi mwengine wa Muslim inasema hivi:
Yule anayetenda kitendo ambacho hakikubaliani na jambo letu kitakataliwa.
**********************
Hadithi Ya 06: Hakika Halali Iko Wazi Na Haramu Iko Wazi
الحديث السادس
"إن الحلال بين وإن الحرام بين"
عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُما قَالَ : سمعتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:
(( إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ وَبَيْنَهُما أمورٌ مُشْتَبِهَاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثيِرٌ مِنَ الناسِ، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ فَقَد اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ في الشَّبُهاتِ وَقَعَ في الْحَرَامِ، كالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ، أَلا وَإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمىً أَلا وَإنَّ حِمَى الله مَحَارِمُه، أَلا وَإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً إذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ وإذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلا وَهِيَ الْقَلْبُ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
HADITHI YA 6
HAKIKA HALALI IKO WAZI NA HARAMU IKO WAZI
Kutoka kwa Abu Abdullah An-Nu’uman Ibn Bashiyr رضي الله عنه ambaye alisema: Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema:
Halali iko wazi na haramu iko wazi, baina yao ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawajui. Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchunga anayechunga pembezoni mwa mpaka, mara huingia ndani (ya shamba la mtu). Hakika kila mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya Allaah سبحانه وتعالى ni makatazo Yake. Na hakika katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama kikitangamaa, kiwiliwili chote kitakua kizima, kikharibika kiwiliwili chote huharibika. Basi jua (kipande hicho cha nyama) ni moyo.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
**********************
Hadithi Ya 07: Dini Ni Nasiha
الحديث السابع
"الدين النصيحة"
عن أبي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بنِ أوْسٍ الدَّارِيِّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلم قالَ:((الدِّينُ النَّصِيحَةُ)). قُلْنَا: لِمَنْ ؟ قالَ: ((للهِ، ولِكِتَابِهِ، ولِرَسُولِهِ، ولِلأَئِمةِ المُسْلِمِينَ، وعامَّتِهِمْ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 7
DINI NI NASIHA
Kutoka kwa Abu Ruqayyah Tamim Ibn Aus Addarryرضي الله عنه ambaye amesema kuwa Bwana Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Dini ni nasiha. Tukauliza: Kwa nani? Akasema kwa Allaah (Kukiri Uungu wake na kwamba Hana mshirika), Kitabu chake (Kukubali kuwa ni maneno ya Allah yasiyo na shaka), na Mtume wake (Kumkubali na kukubali ujumbe aliotumwa nao), na kwa Viongozi wa Waislamu (Kuwatii na kuwafuata katika mema na kuwaasa katika yale wanayokwenda nayo kinyume), na watu wa kawaida (kuusiana mema na kukatazana mabaya kwa njia nzuri).
Imesimuliwa na Muslim
Hadithi Ya 08: Nimeamrishwa Nipigane Na Watu
الحديث الثامن
"أمرت أن أقاتل الناس"
عن ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أنَّ رسُوَل الله صلى الله عليه وسلم قال: ((أُمِرْتُ أَنْ أُقاتِلَ النَّاسَ حتَّى يَشْهَدُوا أنْ لا إلَهَ إلاَّ اللهُ وأنَّ محمداً رسوُل اللهِ، ويُقِيمُوا الصَّلاَةَ، ويُؤتُوا الزَّكاةَ، فإذا فَعَلوا ذَلِكَ عَصَموا منِّي دِماءَهُمْ وأمْوَالَهُمْ إلا بِحَقِّ الإِسْلامِ، وحِسابُهُم على اللهِ تعالى))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
HADITHI YA 8
NIMEAMRISHWA NIPIGANE NA WATU
Kutoka kwa Ibn ‘Umar رضي الله عنهما ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema :
Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washahadie kuwa hakuna Mungu ispokuwa Allaah سبحانه وتعالى na Muhammad ni Mjumbe wa Allaah سبحانه وتعالى na mpaka watakaposwali, na wakatoa zaka, na wakifanya hivyo, watakuwa wamepata himaya kwangu ya damu yao, na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislamu. Na hesabu yao itakuwa kwa Allaah سبحانه وتعالى .
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
**********************
Hadithi Ya 09: Nilichokukatazeni Kiepukeni
الحديث التاسع
"ما نهيتكم عنه فاجتنبوه"
عن أبي هُرَيْرةَ عَبْدِ الرَّحمنِ بنِ صَخْرٍ رضي الله عنه قال : سمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((ما نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ فَاجتَنبوهُ، وَمَا أَمَرْتُكُمْ بِهِ فأتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ، فإنَّما أَهْلَكَ الَّذينَ مِنْ قَبْلِكُمْ كَثْرَةُ مَسَائِلِهِمْ واخْتلاُفُهُمْ على أَنْبِيَائِهِمْ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
HADITHI YA 9
NILICHOKUKATAZENI KIEPUKENI
Kutoka kwa Abu Hurayra Abdur Rahman Ibn Sakhr رضي الله عنه ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Kile nilichokukatazeni kiepukeni, Na kile nilichokuamrisheni fanyeni kwa wingi kadiri muwezavyo. Hakika kilichowaangamiza watu wa Umma zilizopita, ni masuala (mahojiano) mengi na kupingana na Mitume yao .
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
**********************
Hadithi Ya 10: Allaah سبحانه وتعالى Ni Mwema Anakubali Kilicho Chema Tu
الحديث العاشر
"إن الله طيب لا يقبل إلا طيبا"
عن أبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قاَل رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((إنَ الله تعالى طَيِّبٌ لا يَقْبَلُ إلا طَيِّباً، وإنَّ الله أَمَرَ المُؤمِنينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ المُرْسَلينَ فقال تعالى: {يا أَيُّها الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيَّباتِ واعمَلُوا صالحاً} [المؤمنون: 51] وقال تعالى: {يا أَيُّها الَّذِينَ آمَنُوا كلُوا مِنْ طَيِّباتِ ما رَزَقْناكُمْ} [البقرة: 172] ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أشْعَثَ أَغْبَرَ يَمُدُّ يَدَيْهِ إلى السَّماءِ يا رَبُّ يا رَبُّ، ومَطْعَمُهُ حَرَامٌ، ومَشْربُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ وغُذِّيَ بالحَرَامِ، فأَنَّى يُسْتَجَابُ لهُ!)).
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA10
ALLAAH سبحانه وتعالى NI MWEMA ANAKUBALI KILICHO CHEMA TU.
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Allaah سبحانه وتعالى ni Mwema na anakubali kilicho chema tu.
Allaah سبحانه وتعالى ameamrisha Waislamu kufanya yale aliyowaamrisha Mitume, na Yeye سبحانه وتعالى kasema "Enyi Mitume Kuleni katika vitu vyema na mfanye yaliyo sawa" . Allaah سبحانه وتعالىakasema :" Enyi mlioamini kuleni katika vitu vyema ambavyo tumekuruzukuni” Kisha akataja (kisa cha yule) mtu aliyesafiri safari ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku anayanyua mikono yake mbinguni akisema "Ewe Mola! Ewe Mola! Nipe kadhaa, nikinge na kadhaa wakati chakula chake cha haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na kivazi chake ni cha haramu, na anashibishwa na haramu, je, vipi atajibiwa (dua zake?)
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
**********************
Hadithi Ya 11: Wacha Kile Kinachokutia Shaka Ufuate Kile
الحديث الحادي عشر
" دع ما يريبك إلى ما لا يريبك"
عَنْ أَبي مُحمَّدٍ الحسَنِ بْنِ عليّ بْنِ أبي طَالِب، سِبْطِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَرَيْحَانَتِهِ رضيَ اللهُ عنهُما، قالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ ما يَرِيبُكَ إلى مَا لاَ يَرِيُبكَ ))
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَالنَّسَائِيُّ وَقَالَ التِّرْمِذِيُّ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
HADITHI YA 11
WACHA KILE KINACHOKUTIA SHAKA UFUATE KILE
KISICHOKUTIA SHAKA
Kutoka kwa Abu Muhammad Al-Hasan Ibn ‘Ali Ibn Abi Twaalib mjukuu wa Mtume صلى الله عليه وسلم na kipenzi chake رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا alisema :
Nilihifadhi kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم maneno haya: “Wacha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka”.
Imesimuliwa na At-Tirmidhi na An-Nasai, At-Tirmidhi akisema kuwa ni hadithi Hasan na Sahihi.
Hadithi Ya 12 Muislamu Mzuri
الحديث الثاني عشر
"من حسن إسلام المرء"
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مِنْ حُسْنِ إسْلاَمِ الْمَرْءِ تَرْكُهُ مَا لاَ يَعْنِيهِ))
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ ،وَ غَيره هكذا
HADITHI YA12
MUISLAMU MZURI
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye amesema: “Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم: Moja ya sifa nzuri za Muislamu ni kutoshughulika na yale yasiyomuhusu.”
Hadithi iliyo katika daraja ya Hasan (nzuri inayokubalika) Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na wengineo
Hadithi Ya 13: Hatoamini Mmojawenu…
الحديث الثالث عشر
"لا يؤمن أحدكم حتى يحب لأخيه ما يحب لنفسه"
عن أبي حَمْزَةَ أَنسِ بنِ مالكٍ رضي اللهُ عنه خادِمِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم , عَنِ النَّبِي صلى الله عليه وسلم قال : ((لا يُؤمِنُ أحَدُكُمْ حتى يُحِبَّ لأخِيهِ ما يُحِبُّ لِنَفْسِهِ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ .
HADITHI YA 13
HATOAMINI MMOJAWENU…
Kutoka kwa Abu Hamza Anas Ibn Malik رضي الله عنه mtumishi wa Mtume صلى الله عليه وسلم alisema kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Haamini mmoja wenu (kikwelikweli) mpaka atakapompendelea ndugu yake kile anachojipendelea nafsi yake.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
Hadithi Ya 14: Damu Ya Muislamu Isimwagwe Isipokuwa Kwa Sababu Tatu
الحديث الرابع عشر
" لا يحل دم امريء مسلم إلا بإحدى ثلاث"
عن ابْنِ مَسْعُودٍ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ: الثَّيِّبُ الزَّاني، وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ، وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ)).
رَوَاهُ الْبُخَارِيّ وَمُسْلِمٌ
HADITHI YA 14
DAMU YA MUISLAMU ISIMWAGWE ISIPOKUWA KWA SABABU TATU
Kutoka kwa Ibn Mas'udرضي الله عنه ambae alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema :
Damu ya Muislamu haiwezi kwa haki kumwagwa isipokuwa katika hali tatu: Mzinzi Muolewa (Mtu mzima aliyeoa/olewa), uhai kwa uhai (nafsi kwa nafsi) na kwa yule anaewacha dini na akajifarikisha na jamaa (kundi) (amejitenga na watu wa dini yake).
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
Hadithi Ya 15: Aliyekuwa Amemuamini Allaah سبحانه وتعالى Na Siku Ya Qiyaamah Aseme Ya Kheri
الحديث الخامس عشر
"من كان يؤمن بالله واليوم الآخر فليقل خيرا"
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنهُ: أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : ((مَنْ كانَ يُؤمِنُ باللهِ والْيَوْمِ الآخِرِ فَلْيَقُل خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ، ومَنْ كانَ يُؤمِنُ باللهِ والْيَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ جارَهُ، ومَنْ كانَ يُؤمِنُ باللهِ والْيوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
HADITHI YA 15
ALIYEKUWA AMEMUAMINI ALLAAH سبحانه وتعالى NA SIKU YA QIYAAMAH
ASEME YA KHERI
Kutoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye alisema: Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم :
Aliyekuwa amemuamini Allaah سبحانه وتعالى na siku ya Qiyaamah aseme (mambo ya) kheri, au anyamaze, na yule anaemuamini Allaah سبحانه وتعالى na siku ya Qiyaamah awe Mkarimu kwa jirani yake, na yule anaemuamini Allaah سبحانه وتعالى na siku ya Qiyaamah amkirimu mgeni wake.
Imesimuliwa na: Al-Bukhaariy na Muslim
Hadithi Ya 16: Usihamaki
الحديث السادس عشر
" لا تغضب"
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي اللهُ عنه أنَّ رَجُلاً قال لِلنَّبِّي صلى الله عليه وسلم: أَوصِني، قالَ:
((لا تَغْضَبْ))، فَرَدَّدَ مِرَاراً، قال: ((لا تَغْضَبْ)).
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA16
USIHAMAKI
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye amesema:
Mtu alimwambia Mtume صلى الله عليه وسلم Niusie: “akamwambia “usihamaki, yule mtu akakariri tena (ombi lake) mara nyingi, na akamwambia (jizuie) usihamaki.”
Imesimuliwa na Al-Bukhari
Hadithi Ya 17: Mola Kaandika Uzuri (wema) Katika Kila Kitu
الحديث السابع عشر
"إن الله كتب الإحسان على كل شيء"
عن أبي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رضي اللهُ عنه، عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ اللهَ كَتَبَ الإِحْسانَ على كلِّ شَيءٍ، فإذا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذِّبْحَةَ، ولْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ ولْيُرِحْ ذَبيحَتَهُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 17
MOLA KAANDIKA UZURI (WEMA) KATIKA KILA KITU
Kutoka kwa Abu Ya’ala Shaddad Ibn Aws رضي الله عنه ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Mola kaamrisha wema katika kila kitu. Kwa hiyo unapoua (mnyama), ua vizuri na unapochinja chinja vizuri. Basi kila mmoja wenu anoe kisu chake barabara (anapotaka kuchinja) na amuondoshee machungu (asimtese) yule mnyama anayemchinja.
Imesimuliwa na Muslim
Hadithi Ya 18: Mche Mwenyeezi Mungu Popote Ulipo
الحديث الثامن عشر
"اتق الله حيثما كنت"
عن أبي ذَرٍّ جُنْدُب بِن جُنَادَة، وأبي عبد الرحمن مُعَاذ بِن جَبَلٍ رضي الله عنهما، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((اتَّقِ اللهَ حَيْثُما كنْتَ، وأَتْبِعِ السَّيئةَ الحسنةَ تَمْحُها، وخالقِ الناسَ بخُلُقٍ حسنٍ)).
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ، وَفِي بَعْضِ النُّسَخِ: حَسَنٌ صَحِيحٌ.
HADITHI YA 18
MCHE MWENYEEZI MUNGU POPOTE ULIPO
Kutoka kwa Abu Dharr Jundub Ibn Junaada na Abu Abdur Rahmaan
Mu'adh Ibn Jabal رضي الله عنهما ambao wamemnukuu Mtume صلى الله عليه وسلم akisema:
“Mche Allaah سبحانه وتعالى popote pale ulipo na fuatisha kitendo kibaya kwa kitendo kizuri kitafuta (kitendo kibaya) na ishi na watu kwa uzuri.”
Imesimuliwa na At-Tirmidhi na kasema kuwa ni hadithi Hasan na katika maandiko mengine imesemwa kuwa ni Hasan Sahihi
Hadithi Ya 19: Muhifadhi Allaah سبحانه وتعالى Atakuhifadhi
الحديث التاسع عشر
" احفظ الله يحفظك"
عن أبي العَبَّاس عَبْدِ اللهِ بنِ عَبَّاسٍ رَضي اللهُ عنهما قال: كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يًوْماً، فقال: (( يا غُلامُ، إنِّي أُعَلِّمُكَ كلِماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجاهَك، إذا سأَلْتَ فاسْأَلِ اللهَ، وإذا اسْتَعنْتَ فاسْتَعِنْ باللهِ، واعْلَمْ أنَّ الأُمَّة لَوِ اجْتَمَعَتْ على أَنْ يَنْفَعُـوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيْءٍ قدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وإن اجْتَمَعُوا على أن يَضُرَّوكَ بِشيءٍ لَمْ يَضُروكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأقْلامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ ))
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
وَفِي رِوَايَةِ غَيْرِ التِّرْمِذِيِّ:
(( احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ أَمَامَكَ تَعَرَّفْ إِلى اللهِ فِي الرَّخَاءِ يَعْرِفْكَ فِي الشِّدَّةِ واعْلَمْ أَنَ مَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبَكَ وَما أَصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ وَاعْلَمْ أنَ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ وَ أَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرَاً ))
HADITHI YA 19
MUHIFADHI ALLAAH سبحانه وتعالى ATAKUHIFADHI
Kutoka kwa Abul ‘Abbaas Abdullah Ibn ‘Abbaas رضي الله عنهما ambaye alisema:
Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume صلى الله عليه وسلم akaniambia: Kijana nitakufundisha maneno (ya kufaa); Mhifadhi Allaah سبحانه وتعالى (fuata maamrisho Yake na chunga Mipaka Yake) Atakuhifadhi. Muhifadhi Allaah سبحانه وتعالى na utamkuta mbele yako. Ukiomba, muombe Allaah سبحانه وتعالى, ukitafuta msaada tafuta kwa Allaah سبحانه وتعالى. (lazima) ujue kuwa ikiwa taifa zima litaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile alichokwishakuandikia Allaah سبحانه وتعالى na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hotodhurika ila tu kwa kile Allaah سبحانه وتعالىalichokwishakuandikia (kuwa kitakudhuru) . Kwani Kalamu zimeshanyanyuliwa (kila kitu kishaandikwa) na sahifa zimeshakauka (Hakuna kupangwa tena wala kupanguliwa).
Imesimuliwa na At-Tirmidhi akasema kuwa ni hadithi Hasan Sahihi.
Na kwa mapokezi mengine yasiyokuwa ya At-Tirmidhi inasema:
Muhifadhi Allaah سبحانه وتعالى utakuta katangulia mbele yako (kwa ulinzi Wake, himaya na msaada Wake). Mjue Mola wako katika neema (muombe, mche, mtii) Atakujua katika shida (unapokuwa katika dhiki Naye Atakusaidia). Jua kuwa yaliyokukosa hayakuwa yakupate na yaliokupata hayakuwa yakukose. Jua kuwa ushindi uko pamoja na subira, na faraja iko pamoja na dhiki, na raha iko pamoja na shida (haviachani).
Hadithi Ya 20: Ikiwa Huna Haya Basi Fanya Utakavyo
الحديث العشرون
"إذا لم تستح فاصنع ما شئت"
عن أبي مَسْعُودٍ عُقْبَةَ بن عمرو الأَنْصَارِيّ البَدْرِيّ رضي اللهُ عنه قال : قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّ مما أَدْرَكَ النَّاسُ مِنْ كَلامِ النُّبُوَّةِ الأولَى: إِذا لمْ تَسْتَحِ فاصْنَعْ ما شِئْتَ)).
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 20
IKIWA HUNA HAYA BASI FANYA UTAKAVYO
Kutoka kwa Abu Mas'ud ‘Uqbah Ibn 'Amr Al Ansariy Al Badriy رضي الله عنه ambaye amesema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: “Katika maneno ambayo watu waliyapata kutoka kwa Mitume wa mwanzo (waliotangulia) ni haya: “Ikiwa huna haya basi fanya utakalo.”
Imesimuliwa na Al-Bukhari
Hadithi Ya 21: Sema Namuamini Allah Kisha Kuwa Mwenye Msimamo
الحديث الحادي والعشرون
"قل آمنت بالله ثم استقم"
عن أبي عَمْرو، وَقِيلَ: أبي عَمْرَةَ، سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللهِ رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَال: قُلْتُ: يا رَسُولَ الله، قُلْ لي في الإِسْلاَمِ قَوْلاً، لاَ أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَداً غَيْرَكَ. قَال: ((قُلْ: آمَنْتُ باللهِ ثُمَّ اسْتَقِمْ)).
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 21
SEMA NAMUAMINI ALLAH KISHA KUWA MWENYE MSIMAMO
Kutoka kwa Abu 'Amr, vile vile (anajulikana kama ) Abu 'Amra Sufyaan Ibn Abdillah رضي الله عنه ambaye amesema:
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, niambie kitu kuhusu Uislamu ambacho siwezi kumuuliza mtu yeyote ila wewe. Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم ) : Sema; Namuamini Allaah , kisha kuwa mwenye kunyooka. (kwa kuendelea kufanya ibada na kuwa na msimamo madhubuti katika dini)
Imesimuliwa na Muslim.
Hadithi Ya 22: Je, Nikiswali Swalah Za Fardhi, Nikafunga Ramadhaan…
الحديث الثاني والعشرون
"أرأيت إذا صليت المكتوبات وصمت رمضان"
عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ الأنْصَارِيِّ رَضي اللهُ عَنْهُما أَنَّ رَجُلاً سَأَلَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَقال: أَرَأَيْتَ إذَا صَلَّيْتُ الْمكْتُوباتِ، وَصُمْتُ رَمَضانَ، وَأَحْلَلْتُ الْحَلاَلَ، وَحَرَّمْتُ الْحَرَامَ، وَلَمْ أَزِدْ على ذِلكَ شَيْئاً، أَأَدْخُلُ الْجَنَّةَ ؟ قال: ((نَعَمْ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 22
JE, NIKISWALI SWALAH ZA FARDHI, NIKAFUNGA RAMADHAAN…
Inatoka kwa Abu 'Abdillaah Jaabir bin 'Abdillaah Al-Answaariy رضي الله عنه alisema:
Mtu alimuuliza Mtume ,صلى الله عليه وسلم Unafikiri nikiswali Swalah za fardhi, nikafunga Ramadhaan, nikafanya halali kilicho halali na nikaharimisha kile kilichoharimishwa, na nisifanye jambo lolote lingine, je? Nitaingia peponi? Mtume صلى الله عليه وسلم akamjibu: Ndio.
Imesimuliwa na Muslim
Hadithi Ya 23: Tohara Ni Nusu Ya Imaan
الحديث الثالث والعشرون
"االطهور شطر الإيمان"
عن أبي مالكٍ الحارِثِ بنِ عاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رضي اللهُ عنهُ قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيَمانِ، والحمدُ لِلهِ تَمْلأُ الْمِيزَانَ، وسُبْحانَ اللهِ والحمدُ لِلهِ تَمْلآنِ - أو تَمْلأُ - ما بَيْنَ السَّمآءِ والأرضِ، والصَّلاةُ نورٌ، والصَّدَقَةُ بُرْهانٌ، والصَّبْرُ ضِيَاءٌ، والْقُرآنُ حُجَّةٌ لَكَ أو عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدو، فَبائعٌ نَفْسَهُ، فَمُعْتِقُها أَو مُوبِقُها))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 23
TOHARA NI NUSU YA IMAAN
Kutoka kwa Abu Malik Al-Harith Ibn 'Asim Al-Ash'ariyy رضي الله عنه alisema, kasema Mtume wa Allahصلى الله عليه وسلم
Tohara ni nusu ya Imaan. Na AlhamduliLlahi inajaza mizani, na SubhaanaAllah Wal-hamduliLlah inajaza baina ya mbingu na ardhi. Swala ni nuru, Sadaka ni ushuhuda, Subira ni mwangaza, na Qur'aan ni hoja yako au dhidi yako. Kila mtu anaianza siku yake akiichuuza nafsi yake, aidha huiacha huru au anaisambaratisha.
Imesimuliwa na Muslim
Hadithi Ya 24: Enyi Waja Wangu Nimeikataza Nafsi Yangu Dhulma
الحديث الرابع والعشرون
"يا عبادي إني حرمت الظلم على نفسي"
عن أبي ذَرٍّ الْغِفاريِّ رضي الله عنه، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم فيما يَرْويهِ عن رَبِّهِ عَزَّ وجَلَّ أَنَّهُ قال:
(( يا عِبادي إنِّي حَرَّمْتُ الظُلْمَ على نَفْسِي وَ جعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّماً فلا تَظَالَمُوا.
يا عِبادي كُلُّكُمْ ضالٌّ إلا مَنْ هَدَيْتُهُ، فاسْتَهدُوني أهْدِكُمْ.
يا عِبادِي كُلُّكُمْ جائعٌ إلا مَنْ أطْعَمْتُهُ، فاسْتَطْعِمُوني أُطْعِمْكُم.
يا عِبادِي كُلُّكُمْ عَارٍ إلا مَنْ كَسَوْتُهُ، فاسْتكْسوني أَكسُكُم.
يا عِبادِي إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بالليْلِ والنَّهارِ، وأنا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَميعاً، فاسْتَغْفِرُوني أُغْفِر لكُمْ.
يا عِبادِي إِنَّكُمْ لنْ تبْلغُوا ضُرِّي فتَضُرُّوني، ولن تبْلُغُوا نفْعي فَتَنْفعُوني.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ واحدٍ مِنْكُمْ ما زادَ ذلك في مُلْكي شَيئاً.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحدٍ مِنْكُمْ ما نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكي شَيئاً.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجنَّكُمْ قاموا في صَعِيدٍ وَاحِدٍ، فَسَأَلُوني، فأَعْطَيْتُ كلَّ واحدٍ مَسْأَلَتَهُ ما نَقَصَ ذلك مِمَّا عِنْدِي إلا كما يَنْقُصُ الْمِخْيَطُ إذا أُدْخِلَ الْبَحْرَ.
يا عِبادِي إنَّما هي أعمَالُكُمْ أُحْصِيها لَكُمْ ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إيَّاها، فَمَنْ وَجَدَ خيْراً فَلْيَحْمَدِ اللهَ، ومَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذلك فَلا يَلومَنَّ إلا نَفْسَه))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 24
ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA
Kutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifariy رضي الله عنه naye kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم akisimulia yale aliyopokea kutoka kwa Bwana wake عَزَّ وَجَلَّ ni:
Enyi waja Wangu, Nimeikataza nafsi Yangu dhulma na Nimeiharamisha kwenu (hiyo dhulma), kwa hivyo msidhulumiane.
Enyi waja Wangu, nyote mumepotea isipokuwa wale Niliowaongoza, kwa hivyo tafuteni muongozo kutoka Kwangu Nitakuongozeni.
Enyi waja Wangu nyote mna njaa isipokuwa wale Niliowalisha, kwa hivyo tafuteni chakula kutoka Kwangu na Nitakulisheni.
Enyi waja Wangu, nyote muko uchi isipokuwa wale niliowavika nguo, kwa hivyo tafuteni vazi kutoka Kwangu nitakuvisheni.
Enyi waja Wangu, mnafanya makosa usiku na mchana, na ninasamehe dhambi zote, kwa hivyo tafuteni msamaha kutoka Kwangu nitakusameheni.
Enyi waja Wangu hamuwezi kunidhuru Mimi wala kuninufaisha.
Enyi waja Wangu, ingekuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mcha Mungu kama moyo wa mcha Mungu yeyote katika nyinyi, haitaongeza chochote katika ufalme Wangu.
Enyi waja Wangu, angelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mbaya kama moyo mbaya wa mtu miongoni mwenu (mtu mbaya kupita kiasi) haitonipunguzia chochote katika ufalme Wangu.
Enyi waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi mukasimama pahala pamoja na mkaniomba, na nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovya.
Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu ninavyovihesabu, kwa ajili yenu nikakulipeni. Kwa hivyo anayekuta wema amshukuru Allaah na yule anayekuta yasiokuwa mema (basi) ajilaumu mwenyewe.
Imesimuliwa na Muslim
Hadithi Ya 25: Wenye Mali Wameondoka Na Fungu (jaza) Kubwa
الحديث الخامس والعشرون
"ذهب أهل الدثور بالأجور "
عن أبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ ناساً من أَصْحابِ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالوا لِلنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: يا رسولَ اللهِ، ذَهَب أَهْلُ الدُّثورِ بالأُجورِ، يُصَلُّونَ كما نُصَلِّي، ويَصُومُونَ كما نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أَمْوَالِهِمْ. قَالَ: ((أوَ لَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ ؟ إنَّ بكلِّ تَسْبيحَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأَمْرٍ بِالْمَعرُوفِ صَدَقَةً، وَنَهْيٍ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةً، وفي بُضْعِ أحَدِكُمْ صَدَقَةً)). قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأْتي أحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجرٌ ؟ قَالَ:
((أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَها في حَرَامٍ، أَكَانَ عَليْهِ وزْرٌ ؟ فَكَذلِكَ إذَا وَضَعَها في الْحَلاَلِ كانَ لَهُ أَجْرٌ ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 25
WENYE MALI WAMEONDOKA NA FUNGU (JAZA) KUBWA
Kutoka kwa Abu Dharr رضي الله عنه ambaye amesema:
Baadhi ya Maswahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم walimuambia Mtume صلى الله عليه وسلم : Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, wenye mali wameondoka na fungu (jaza) kubwa, wanaswali kama sisi, wanafunga kama sisi, na wanatoa sadaka ya ziyada ya mali zao. Mtume صلى الله عليه وسلم akasema: Mwenyeezi Mungu hajakufanyieni vitu kwa ajili yenu kutoa sadaka? (Basi jueni) Hakika kila Tasbihi (Subhana Allah) ni sadaka, kila Takbiri (Allahu Akbar) ni sadaka, kila Tahmidi (AlhamduliLlah) ni sadaka, na kila Tahlili (Laa ilaaha illa Allaah) ni sadaka, na kulingania jambo jema ni sadaka, na kukataza mabaya ni sadaka na katika kujamii (wake zenu) kila mmoja katika nyinyi ni sadaka. Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume صلى الله عليه وسل mtu anapojitosheleza shahawa yake atapata malipo kwa ajili yake? Akasema صلى الله عليه وسلم : Mnadhani ingekuwa anajitosheleza kwa njia ya haramu angelipata dhambi? Na hivyo ikiwa kafanya kwa njia ya halali basi atapata thawabu.
Imesimuliwa na Muslim
Hadithi Ya 26: Kila Kiungo Cha Mtu Lazima Kitolewe Sadaka
الحديث السادس والعشرون
"كل سلامى من الناس عليه صدقة"
عن أَبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((كُلُّ سُلامَى مِنَ النَّاسِ عليه صَدَقَةٌ، كُلُّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ: تَعْدِلُ بَيْنَ اثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وتُعينُ الرَّجُلَ في دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْها أو تَرْفَعُ لهُ عَلَيْها متَاَعَهُ صَدَقَةٌ، والْكَلِمةُ الطَّيِّبةُ صَدَقَةٌ، وبكُلِّ خَطْوَةٍ تَمشِيها إلى الصَّلاةِ صَدَقَةٌ، وتُمِيطُ الأَذَى عنِ الطَّرِيِق صَدَقَةٌ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
HADITHI YA 26
KILA KIUNGO CHA MTU LAZIMA KITOLEWE SADAKA
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye alisema : Mtume صلى الله عليه وسلم kasema :
Kila kiungo cha mtu lazima kitolewe sadaka kila siku jua inapochomoza, kufanya haki (uadilifu) baina ya watu wawili ni sadaka, kumsaidia mtu kupanda (mnyama) kwa kumsaidia kumnyanyua au kumnyanyulia mizigo yake ni sadaka, neno jema ni sadaka, kila hatua unayokwenda kuswali ni sadaka, kuondosha dhara katika njia ni sadaka.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
Hadithi Ya 27: Uadilifu Ni Tabia Nzuri
الحديث السابع والعشرون
"البر حسن الخلق"
عن النّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ رضيَ اللهُ عَنْهُ عن النَّبي صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((الْبِرُّ حُسْنُ الْخُلُقِ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في نَفْسِكَ وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ .
وعن وَابصَةَ بْنِ مَعْبَدٍ رضي اللهُ عَنْهُ قالَ: قالَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ((جِئْتَ تَسأَلُ عَنِ الْبِرِّ؟)) . قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: ((اسْتَفْتِ قَلْبَكَ، الْبِرُّ مَا اطْمَأَنَّتْ إلَيْهِ النَّفْسُ وَاطْمَأَنَّ إلَيْهِ الْقَلْبُ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في النَّفْسِ وَتَردَّدَ في الصَّدْرِ وَإنْ أَفْتَاكَ النّاسُ وَأَفْتَوْكَ))
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَيْنَاهُ في مُسْنَدَي الْإِمَامَيْنِ أَحْمَدَ بْنِ حَنْبَلٍ وَالدَّارِمِيّ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ.
HADITHI YA 27
UADILIFU NI TABIA NZURI
Kutoka kwa An-Nawwaas Ibn Sam'aan رضي الله عنه ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Uadilifu ni tabia nzuri na udhalimu ni kile kitu ambacho huyumbayumba (chenye mashaka) katika nafsi yako na hupendelei watu kukitambua.
Imesimuliwa na Muslim
Na kutoka kwa Waabisah Ibn Ma'abad رضي الله عنه ambaye alisema:
Nilikuja kwa Mtume صلى الله عليه وسلم naye akasema:
Umekuja kuuliza juu uadilifu? Nikasema: Ndio . Akasema: Ushaurishe moyo wako. Uadilifu ni kile ambacho nafsi yako inakihisi shwari na moyo wako pia unahisi shwari, na udhalimu ni kile kinachoyumbayumba katika nafsi na kwenda na kurudi kifuani ijapokuwa watu wamekupa shauri lao la kisheria (kukipendelea).
Hadithi Ya 28: Nakuusieni Kumcha Allaah Na Tabia Njema
الحديث الثامن والعشرون
"أوصيكم بتقوى الله وحسن الخلق"
عن أبي نَجيحٍ الْعِرْباضِ بنِ سارِيَةَ رضي اللهِ عنه قال: وَعَظَنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنها الْقُلُوبُ، وذَرَفَتْ منها الْعُيُونُ، فَقُلْنا: يا رسول اللهِ، كأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ، فأَوْصِنا. قال:
((أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ عَزَّ وَجَلَّ، والسَّمْعِ والطَّاعَةِ، وإن تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فإنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلافاً كَثِيراً، فَعَليْكُمْ بِسُنَّتي وسُنَّةِ الخُلفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيِّينَ، عَضُّوا عَلَيْها بالنَّواجِذِ، وإيَّاكُمْ ومُحْدَثاتِ الأُمُورِ، فإنَّ كلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ وَ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلاَلَةٌ وَكُلَّ ضَلاَلَةٍ فِي النَّارِ))
رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
HADITHI YA. 28
NAKUUSIENI KUMCHA ALLAAH NA TABIA NJEMA
Kutoka kwa Abu Najiih Al 'Irbaadh Ibn Saariyah رضي الله عنه ambaye alisema kwamba:
Mtume صلى الله عليه وسلم alituhutubia hutuba ambayo nyoyo zetu zilijaa hofu na macho yetu yalitutoka machozi. Tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu!, inaonyesha kama kwamba hii ni hutuba ya kuaga, kwa hivyo tuusie. Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم ) nakuusieni kumcha Allaah سبحانه وتعالى na kumtii kiongozi wenu hata akiwa mtumwa. Yule atakayeishi (muda mrefu) ataona ikhtilaaf nyingi (migongano), kwa hivyo fuateni mwendo wangu (Sunnah) na mwendo wa Makhalifa walioongoka (Makhalifa wanne). Shikamaneni nazo kwa magego (kwa nguvu). Na tahadharini na mambo mapya yanayozuliwa kwani kila jambo jipya ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu, na kila upotofu unapeleka motoni.
Imesimuliwa na Abu Dawuud na At Tirmidhi na wamesema ni Hadithi Hasan na Sahihi.
Hadithi Ya 29: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote
الحديث التاسع والعشرون
"تعبد الله لا تشرك به شيئا"
عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ : تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ ،وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ)) .ثم قال: (( ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟: الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ، وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: {تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ} - حتى بلغ - {يَعْمَلُونَ} السجدة: 16-17 .
ثم قال: ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال: (( رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ )).
ثم قال: (( ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال: ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا)) . قلت : يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه ؟)) فقال: (( ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ, وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على وُجُوهِهِمْ )) أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ ألسِنَتهم))
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
HADITHI YA 29
MUABUDU ALLAAH NA USIMSHIRIKISHE NA CHOCHOTE
Kutoka kwa Mu'aadh Ibn Jabal رضي الله عنه amesema:
Nilisema: Ewe Mtume صلى الله عليه وسلم , niambie kitendo ambacho kitanipeleka peponi na kitaniokoa na moto. Akasema : Umeniuliza jambo kubwa lakini ni rahisi kwa yule ambae Mola anaemsahilishia. Muabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, Swali, toa Zaka, funga Ramadhani, nenda kuhiji (Makka). Kisha akasema: Je? Nikuonyeshe milango ya kheri? Saumu ni ngao, sadaka inazima dhambi kama vile maji yanavyozima moto, na kuswali katikati ya usiku: Kisha akasoma {Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku. Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda}
Sura As-Sajda 32: 16 na 17
Tena akasema: Je, nikwambie kilele cha hilo jambo; nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa? Nikasema : Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu. Akasema: kilele chake ni Uislamu, nguzo yake ni Swala na sehemu yake ya juu kabisa ni Jihaad. Kisha akasema : Je, nikwambie muhimili wa yote haya? Nikasema: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu. Akaukamata ulimi wake na akasema; Uzuie huu. Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu; yale tunayoyasema tutahukumiwa kwayo? Akasema: mama yako akuhurumie ewe Mu'aadh! Kuna kitu zaidi kinachowaangusha watu kifudifudi motoni kama si mavuno ya ndimi zao?
Imesimuliwa na At-Tirmidhi na ni hadithi Hasan.
Hadithi Ya 30: Allaah Amefaridhisha Mambo Ya Dini Tusiyapuuze
الحديث الثلاثون
"إن الله تعالى فرض فرائض فلا تضيعوها"
عَنْ أَبيِ ثَعْلَبَةَ الخُشَنِيِّ جُرْثُومِ بْن نَاشرٍ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ:
(( إنّ اللهَ تَعَالى فَرَضَ فَرَائِضَ فَلاَ تُضَيّعوهاَ وَحَدَّ حُدُودَاً فَلاتَعْتَدُوهَا وَحَرّمَ أَشْياءَ فَلاَتَنْتَهِكُوهَا وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رَحْمَةً لَكُمْ غَيْرَ نِسْيانٍ فَلا تَبْحَثُوا عَنْهَا ))
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ الدَّارَقُطْنِيّ وَغَيْرُهُ
HADITHI YA 30
ALLAAH AMEFARIDHISHA MAMBO YA DINI TUSIYAPUUZE
Kutoka kwa Abu Tha'alaba Al-Khushani Jurthuum Ibn Naashib رضي الله عنه naye kapokea kwa Mtume صلى الله عليه وسلم :
Allaah سبحانه وتعالى amefaridhisha mambo ya dini kwa hivyo usiyapuuze. Vile vile kaweka mipaka usiikiuke. Amekataza baadhi ya mambo kwa hivyo usifanye. Yale aliyoyanyamazia ni kwa ajili ya huruma zake kwako wala hakusahau kwa hivyo usiyadadisi.
Imesimuliwa na Daaraqutni na wengineo . Hadithi Hasan
Hadithi Ya 31: Upe Ulimwengu Kisogo Allaah Atakupenda
الحديث الحادي والثلاثون
"ازهد في الدنيا يحبك الله"
عَنْ أَبِي العَبّاسِ سَهلِ بْن سَعْدٍ السّاعِدِيِّ رضي الله عنه قَالَ : جَاءَ رَجُلُ إِلى النَبِي صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ . فَقَالَ: (( ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النّاسُ)).
رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَغَيْرُهُ بِأَسَانِيدَ حَسَنَةٍ.
HADITHI YA 31
UPE ULIMWENGU KISOGO ALLAAH ATAKUPENDA
Kutoka kwa Abu Al-‘Abbaas Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiy رضي الله عنه ambaye alisema:
Mtu alikuja kwa Mtume صلى الله عليه وسلم na akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, nielekeze kitendo ambacho nikitenda kitasababisha Mola kunipenda na watu kunipenda. Akasema (صلى الله عليه وسلم ) : Upe ulimwengu kisogo na Mwenyeezi Mungu atakupenda, na jiepushe na mali za watu na watu watakupenda.
Imesimuliwa na Ibn Maajah na wengineo kwa mtiririko mzuri wa mapokezi.*
*Hata hivyo wanachuoni wa Hadiyth wameeleza kuwa Hadiyth hii ni dhaifu kutokana na udhaifu wa sanad yake japo An-Nawawiy kaitumia na kasema ina sanad nzuri.
Hadithi Ya 32: Kusiwe Na Kudhuriana Wala Kulipiza Dhara
الحديث الثاني والثلاثون
"لا ضرر ولا ضرار"
عَنْ أَبىِ سَعيدٍ سَعْدِ بْن مَالكِ بْن سِنَانٍ الْخُدريِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ :(( لاَ ضَرَرَ وَلاَ ضِرَارَ ))
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَالدَّارَقُطْنِيّ، وَغَيْرُهُمَا مُسْنَدًا. وَرَوَاهُ مَالِكٌ فِي "الْمُوَطَّإِ مُرْسَلاً عَنْ عَمْرِو بْنِ يَحْيَى عَنْ أَبِيهِ عَنْ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم مُرْسَلًا، فَأَسْقَطَ أَبَا سَعِيدٍ، وَلَهُ طُرُقٌ يُقَوِّي بَعْضُهَا بَعْضًا.
HADITHI YA 32
KUSIWE NA KUDHURIANA WALA KULIPIZA DHARA
Kutoka kwa Abu Sa'iid Sa'ad Ibn Malik Ibn Sinaan Al-Khudhri رضي الله عنه ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Kusiwe na kudhuriana wala kulipa dhara.
Imesimuliwa na Ibn Maajah, Daaraqutni na wengineo na ina kiwango cha 'Musnad'
Vile vile imesimuliwa na Malik katika (kitabu) Al-Muwatta kama 'Mursal'
Inayo mtiririko wa mapokezi kutoka kwa 'Amr Ibn Yahya, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم hata ukimuacha Abu Sa'id bado inayo mtiririko wa mapokezi unayoiunga mkono.
Hadithi Ya 33: Jukumu La Ushahidi Liko Kwa Yule Anayedai Na Kula Kiapo Kunamuwajibikia Yule Anayekana
الحديث الثالث والثلاثون
"البينة على المدعي واليمين على من أنكر "
عن ابن عَبَّاسٍ رضي اللُه عنهما: أن رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قال: ((لَو يُعْطَى النَّاسُ بِدَعْوَاهُمْ لادَّعَى رِجَالٌ أموالَ قَوْمٍ ودِماءَهُمْ لَكِنِ البَيِّنَةُ على المُدَّعِى والْيَمينُ على من أَنْكَرَ)).
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ الْبَيْهَقِيّ وَغَيْرُهُ هَكَذَا، وَبَعْضُهُ فِي "الصَّحِيحَيْنِ".
HADITHI YA 33
JUKUMU LA USHAHIDI LIKO KWA YULE ANAYEDAI
NA KULA KIAPO KUNAMUWAJIBIKIA YULE ANAYEKANA
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas رضي الله عنه ambaye amesema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم alisema:
Kama watu wangelipewa kwa mujibu wa madai yao, watu wangelidai mali na damu za wenzao (uhai) lakini jukumu la ushahidi liko kwa yule anayedai na kula kiapo kunawajibika kwa yule anayekana (kuwa hajatenda).
Imesimuliwa na Al-Bayhaqi na wengineo. Ni Hadithi Hasan.
Hadithi Ya 34: Yeyote Atakayeona Kitendo Kiovu AkiondoeKwa Mkono Wake
الحديث الرابع والثلاثون
"من رأى منكم منكرا فليغيره بيده"
عن أبي سعيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقوُل :
((مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَراً فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإنْ لمَْ يَسْتَطِعْ فَبلِسانِهِ، فَإنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أضْعَفُ
اْلإِيمَانِ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 34
YEYOTE ATAKAYEONA KITENDO KIOVU AKIONDOE
KWA MKONO WAKE
Kutoka kwa Abu Sa'iid Al-Khudhriy رضي الله عنه ambaye amesema : Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema:
Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu mwache akiondoe (abadilishe) kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kuona baya na kunyamaza) ni udhaifu wa Imani.
Imesimuliwa na Muslim
Hadithi Ya 35: Msioneane Choyo, Msizidishiane Bei, Msichukiane
الحديث الخامس والثلاثون
"لا تحاسدوا ولا تناجشوا ولا تباغضوا"
عن أبي هُريرةَ رضي اللهُ عنه قال: قال رسوُل الله صلى الله عليه وسلم : ((لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا، ولا تَباغَضُوا، ولا تَدَابَرُوا، ولا يَبعْ بَعْضُكُمْ على بَيْعِ بَعْضٍ، وكُونُوا عِبادَ اللهِ إخْوَاناً، المُسْلمُ أَخُو المُسْلمِ: لا يَظْلِمُهُ، ولا يَكْذِبُهُ، ولا يَحْقِرُهُ، التَّقْوَى هاهُنا - ويُشِيرُ إلى صَدْرِه ثَلاثَ مَرَّاتٍ , بِحَسْبِ امْرِىءٍ مِنَ الشَّرِّ أن يَحْقِرَ أخاهُ المُسْلِمَ، كُلُّ المُسْلِمِ على الْمسْلِم حَرَامٌ: دَمُهُ ومالُهُ وعِرْضُهُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 35
MSIONEANE CHOYO, MSIZIDISHIANE BEI, MSICHUKIANE
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambae amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Msioneane choyo, wala msizidishiane bei (za vitu), wala msichukiane, wala msipigane mapande (msitengane), wala msishindane kwa kupunguza bei. Lakini kuweni ndugu, enyi waja wa Mwenyeezi Mungu, Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake, hamdhulumu wala hamvunji, hamwambii uongo wala hamdharau. Ucha Mungu uko hapa (huku akiashiria kifuani kwake kwa vidole vyake) mara tatu. Ni uovu wa kutosha kwa mtu kumdharau ndugu yake Muislamu. Muislamu ameharamishiwa kwa Muislamu mwenzake: damu yake, mali yake na heshima yake (Yaani haramu kuchukua mali ya mwenzako, kumuua na kumdhalilisha).
Imesimuliwa na Muslim
Hadithi Ya 36: Atakayemuondoshea Shida Muislamu Mwenzake,Allah Atamuondoshea Shida Zake
الحديث السادس والثلاثون
"من نفس عن مسلم كربة"
عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال: (( مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ، ومَنْ يَسَّرَ على مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللهُ عليه في الدنْيا والآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في الدُّنْيا والآخِرَةِ واللهُ في عَوْنِ الْعَبْدِ ما كانَ الْعَبْدُ في عَونِ أخيهِ. ومَنْ سلك طَريقاً يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْماً سَهَّلَ اللهُ له بِهِ طَرِيقاً إلى الجنَّةِ.
وَمَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ عِنْدَه . وَمَنْ بَطَّأ بِه عَمَلُهُ لمْ يُسْرِعْ به نَسَبُهُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ بهذا اللفظ.
HADITHI YA 36
ATAKAYEMUONDOSHEA SHIDA MUISLAMU MWENZAKE,
ALLAH ATAMUONDOSHEA SHIDA ZAKE
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye amesema kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Yeyote atakaemuondoshea shida ya kidunia Muislamu mwenzake, Allaah Atamuondoshea moja katika shida za siku ya Kiyama.
Yeyote yule anaemsaidia muhitaji (maskini) Allaah Atamsaidia haja zake hapa duniani na akhera. Yeyote yule anayemsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri hapa duniani na akhera.
Mwenyeezi Mungu humsaidia mja wake wakati wote mja anapomsaidia nduguye (Muislamu). Yeyote yule anayekamata njia kutafuta elimu, Allaah Atamrahisishia njia ya peponi. Hawakutaniki watu katika nyumba ya Mwenyeezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyeezi Mungu na wakasomeshana pamoja ila watashukiwa na utulivu (sakina) na kheri. Rehema (za Allah) huwafunika na Malaika huwazunguka na Allaah Huwakumbuka kwa wale walioko pamoja Nae. Yeyote yule anayeakhirishwa (anayecheleweshwa) na vitendo vyake (kwenda peponi) hatoharakishwa na Nas ab yake.
Imesimuiwa na Muslim
Hadithi Ya 37: Allaah Kaviandika Vitendo Vyema Na Vibaya
الحديث السابع والثلاثون
عَن ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا عَنِ النبي صلى الله عليه وسلم فِيْمَا يَرْوِيْهِ عَنْ رَبِّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالى أَنَّهُ قَالَ:
(إِنَّ الله كَتَبَ الحَسَنَاتِ وَالسَّيئَاتِ ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ؛ فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً،وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِمائَةِ ضِعْفٍ إِلىَ أَضْعَاف كَثِيْرَةٍ. وَإِنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً،وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً)
رَوَاهُ البُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ في صَحِيْحَيْهِمَا بِهَذِهِ الحُرُوْفِ
HADITHI YA 37
ALLAAH KAVIANDIKA VITENDO VYEMA NA VIOVU
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas رضي الله عنهما kapokea kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم amesema kutokana na yale aliyoyapokea kutoka kwa Mola wake Aliyetukuka, kwamba Kasema: ((Hakika Allaah Ameviandika vitendo vyema na viovu, kasha Akavibainisha. Basi atakayeazimia kufanya tendo jema kisha asiweze kulifanya, basi Allaah Atamwandikia ujira wa tendo jema lililokamika. Na ikiwa aliazimia kulifanya kisha akalifanya, basi Allaah Atamwandikia (Atamlipa) ujira mara kumi hadi mara mia saba na zaidi ya idadi hiyo.
Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa herufi hizi
Hadithi Ya 38: Anayeonyesha Uadui Kwa Rafiki Yangu Mtiifu Ninatangaza Vita Dhidi Yake
الحديث الثامن والثلاثون
"من عادى لي وليا فقد آذنته بالحرب"
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قال: قال رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : ((إنَّ الله تَعالَى قَال : مَنْ عَادَى لي وَلِيّاً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُهُ عَلَيْهِ، وَلا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إلَيَّ بِالنَّوَافِلٍ حَتَّى أُحِبَّهُ، فإذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بهِ، وَيَدَهُ الّتي يَبْطِشُ بهَا، وَرِجْلَهُ الّتي يَمْشي بِهَا، وَلَئِنْ سَأَلِني لأعْطِيَنَّهُ، ولَئِن اسْتَعَاذَنِي لأُعِيذَنَّهُ ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 38
ANAYEONYESHA UADUI KWA RAFIKI YANGU MTIIFU
NINATANGAZA VITA DHIDI YAKE
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye amesema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: Allaah سبحانه وتعالى kasema: Anayeonyesha uadui kwa Walii Wangu (rafiki wa karibu, yaani mja mtiifu aliye karibu naye) , nitatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote ninachokipenda zaidi kama zile amali nilizomuwajibisha, na mja Wangu anazidi kukaribia Kwangu kwa amali njema zisizokuwa wajibu ili nimpende. Ninapompenda, Ninakuwa masikio yake anayosikilizia (yaani Allah atamjaalia asikie mazuri kama Qur’an, Dhikr, Mawaidha n.k. Na sio Muziki, Masengenyo, na Machafu mengine), macho yake anayoonea (yaani Allah atamfanya macho yake yawe yanatazama yale ya kheri), mikono yake ambayo anakamatia (Allah atafanya mikono yake ikamate vile vya halali na kufanya yale yanayomridhisha Allah), miguu yake anayoendea (na Allah ataifanya miguu yake isitembee kuyaendea ila yale mema, ya kheri na Atakayoridhika nayo Yeye Allah). Anaponiomba (kitu) bila shaka Ninampa, na anaponiomba ulinzi bila shaka Nitamlinda.
Imesimuliwa na Al-Bukhari
Hadithi Ya 39: Allaah Amewasamehe Umma Wake Kukosea Na Kusahau Kwa Ajili Yake ( Mtume صلى الله عليه وسلم )
الحديث التاسع والثلاثون
"إن الله تجاوز لي عن أمتي الخطأ والنسيان"
عَن ابْنِ عَبَّاسِ رَضِيَ الله عَنْهُما: أن رَسُوَل اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : ((إنَّ الله تَجاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتي: الْخَطَأَ، والنِّسْياَنَ، وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ)).
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَالْبَيْهَقِيّ وَغيرهما
HADITHI YA 39
ALLAAH AMEWASAMEHE UMMA WAKE KUKOSEA NA KUSAHAU KWA AJILI YAKE ( MTUME صلى الله عليه وسلم )
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas رضي الله عنهما ambaye amesema kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Allaah Amewasamehe kwa ajili yangu umma wangu kwa kukosea, kusahau, na yale wanayoyafanya kwa kulazimishwa kwa nguvu (ambayo hawana khiyari nayo).
Imesimuliwa na Ibn Maajah na Al-Bayhaqi
Hadithi Ya 40: Kuwa Duniani Kama Vile Mgeni Au Mpita Njia
الحديث الأربعون
"كن في الدنيا كأنك غريب أو عابر سبيل"
عن ابنِ عُمَرَ رضي اللهُ عنهما قال: أَخَذَ رسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم بِمَنْكِبيَّ فقال : ((كُنْ في الدُّنْيا كأنَّكَ غَرِيبٌ، أو عابرُ سبِيلٍ)).
وكانَ ابنُ عُمَرَ رَضي اللهُ عنهما يقولُ: إذا أمْسَيْتَ فلا تَنْتظِرِ الصبَّاحَ، وإذا أصْبَحْتَ فلا تَنْتَظِرِ الَمسَاءَ، وخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرضِكَ، ومِنْ حَياتِكَ لِمَوْتِكَ.
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 40
KUWA DUNIANI KAMA VILE MGENI AU MPITA NJIA
Kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنهما ambaye alisema:
Mtume صلى الله عليه وسلم alinishika bega na akasema: Kuwa (ishi) duniani kama vile mgeni au mpita njia.
Naye Ibn 'Umar رضي الله عنه alikuwa akisema : Ukishinda hadi jioni usitaraji kuishi mpaka asubuhi, na ukiamka asubuhi usitaraji kuishi mpaka jioni, chukua uzima wako kwa ugonjwa wako (yaani fanya yale yote mema uwezayo wakati bado una afya nzuri kwani siku ukiumwa hutoweza kuyafanya), na uhai wako kwa kifo chako (tumia maisha yako vizuri kwa kufanya amali njema maana ukishafariki hakuna tena uwezalo kulifanya).
Imesimuliwa na Al-Bukhari
Hadithi Ya 41: Hatoamini Mmoja Wenu Mpaka Mapenzi Yake Yatakapomili (yatakapoendana) Na Yale Niliyokuja Nayo
الحديث الحادي والأربعون
"لا يؤمن أحدكم حتى يكون هواه تبعا لما جئت به"
عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بِنْ عَمْرُو بِنْ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم :((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ ))
حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ، رَوَيْنَاهُ فِي كِتَابِ "الْحُجَّةِ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ.
HADITHI YA 41
HATOAMINI MMOJA WENU MPAKA MAPENZI YAKE YATAKAPOMILI (YATAKAPOENDANA) NA YALE NILIYOKUJA NAYO
Kutoka kwa Abu Muhammad Abdullah Ibn 'Amr Bin Al-'As رضي الله عنه ambae alisema : Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Hatokua kaamini (kikwelikweli) mmoja wenu mpaka mapenzi yake yatakapomili (yatakapotii au kuwafikiana) kwenye yale niliyoyaleta (mafundisho).
Hadithi Hasan iliyotoka katika kitabu “Al-Hujjah” ikiwa na mtiriko mzuri wa mapokezi
Hadithi Ya 42: Ewe Mwana Wa Adam, Utakaponiomba Na Kuweka Matumaini Kwangu Basi Nitakusamehe
الحديث الثاني والأربعون
"يا ابن آدم إنك ما دعوتني ورجوتني"
عن أنس رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي. يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ . يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لاَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً))
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
HADITHI YA 42
EWE MWANA WA ADAM, UTAKAPONIOMBA NA KUWEKA MATUMAINI
KWANGU BASI NITAKUSAMEHE
Kutoka kwa Anas رضي الله عنه ambaye alisema : Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema :
Mwenyeezi Mungu amesema : Ewe Mwana wa Adam utakaponiomba na kuweka matumaini kwangu, basi nitakusamehe makosa uliyoyafanya na sitojali. Ewe Mwana wa Adam kama dhambi zako zingefika mawingu ya mbingu na wewe ukaomba msamaha kwangu, ningekusamehe. Ewe Mwana Wa Adam kama ungelinijia na dhambi kubwa kama dunia na ukanikabili bila ya kunishirikisha nitakupa maghfira.
Imesimuliwa na Tirmidhi na kasema ni hadithi Hasan Sahihi
Source URL: http://alhidaaya.com/sw/node/961
No comments:
Post a Comment