Page 1 of 5
BARAZA LA WAKUU WA SHULE ZA KIISLAMU TANZANIA
MTIHANI WA UTAMILIFU WA SHULE ZA KIISLAMU KIDATO IV
ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
(Kwa Watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
MUDA: SAA 3 Ijumaa, 25 Agosti 2023 mchana
Maelekezo
1. Mtihani huu una sehemu tatu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C.
3. Hakikisha unasoma maelekezo ya kila swali kwa umakini.
4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
5. Hakikisha unaandika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha
kujibia.
015
Page 2 of 5
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo
kwenye kijitabu chako cha kujibia.
(i) Umewakuta wanafunzi wa kidato cha kwanza wakibishana juu ya nafasi ya elimu
katika Uislamu. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo inaonesha usahihi wa jambo
wanalobishana?
A. Elimu ndio amri ya kwanza kwa mwanadamu
B. Elimu ya mazingira ndio amri ya kwanza kwa mwanadamu
C. Elimu ya akhera ndio amri ya kwanza kwa mwanadamu
D. Elimu ya swala ndio amri ya kwanza kwa mwanadamu
E. Elimu ya dunia na Akhera ndio nyenzo ya kuwa na maisha mazuri
(ii) Ifahamishe jamii yako kosa walilofanya watu wa Madyan ili wasipate ghadhabu za
Allah duniani na Akhera kati ya haya yafuatayo:
A. Kuchanganya haki na batili
B. Kuabudu masanamu
C. Kujifakharisha
D. Kupunja vipimo
E. Kuua Manabii wa Allah
(iii) Umeombwa usimamie mazishi ya jirani yako Muislamu. Jambo gani utawaongoza
watu kufanya mara tu baada ya kuzika?
A. Kusoma Yaa Siin juu ya kaburi
B. Kulipa madeni ya maiti
C. Kumlakinisha maiti
D. Kumuombea msamaha maiti
E. Kudhikiri kwa adhkar
(iv) Mdogo wako anafanya ibada maalumu huku akicheza kamari, hii ni kwa sababu hajui
uhusiano uliopo kati ya ibada hizo na lengo la maisha yake. Maelezo yapi kati ya
yafuatayo yanaonesha uhusiano huo?
A. Kutekeleza wajibu wa maisha
B. Kujiepusha na moto wa Allah
C. Kufikia lengo la kuumbwa
D. Kufikia hadhi ya Ukhalifa
E. Kupata pepo ya Allah
(v) Ikitokea ndugu yako amekasirika kiasi cha kutaka kumdhuru rafiki yake, utamshauri
afanye nini ili kudhibiti hali hiyo?
A. Amswalie Mtume
B. Alete Takbir
C. Alete Istiadha
D. Alete Bismallah
E. Alete Tahlil
Page 3 of 5
(vi) Mtaani kwenu kumezuka hofu kubwa ya watu kusumbuliwa na wachawi. Utaishauri
nini familia yako kufanya?
A. Kuchoma udi rohani
B. Kuchoma ubani Maka
C. Kusoma muawidhatain
D. Kuweka zindiko mlangoni
E. Kutundika Yaa Siin mlangoni
(vii) Vipengele vipi kati ya vifuatavyo utavitumia kumfahamisha ndugu yako sehemu za
Hadith katika uandishi wake ili aitambue Hadith kamili?
A. Isnad, Matin na Riwaya
B. Matini Rawi na Isnad
C. Riwaya, Rawi na Sanad
D. Sanad, Isnad na Matin
E. Rawahu, Riwaya na Rawi
(viii) Umempa kazi mwanafunzi mwenzio akubainishie sifa za mpokezi wa Hadith
akaorodhesha sifa tano. Sifa hizi zote ni sahihi ISIPOKUWA ipi?
A. Ukweli
B. Uadilifu
C. Udhibitifu
D. Ucha Mungu
E. Umri
(ix) Mzee Tondo anajitahidi kuhudumia familia yake vizuri kwa kuwalisha vizuri,
kuwavisha vizuri, kwa sababu ana kazi inayompatia kipato kizuri. Mzee huyu
ameepukana na Dini gani?
A. Utawa
B. Ukafiri
C. Ushirikina
D. Dini za watu
E. Dini ya Shetani
(x) Bwana Manyasi ni mpiga ramli maarufu. Bwana huyu anakwenda kinyume na Taw-
hid gani?
A. Malezi ya Allah
B. Majina na sifa za Allah
C. Ibada maalumu za Allah
D. Hukumu na sharia za Allah
E. Mamlaka ya Allah.
Page 4 of 5
2. Oanisha mali zinazojuzu kutolewa zakat zilizokidhi vigezo vyote zilizo katika Orodha A na
viwango vinavyostahiki kutolewa vilivyo katika Orodha B kisha jaza herufi ya jibu sahihi
katika kijitabu chako cha kujibia.
ORODHA A ORODHA B
(i) Dhahabu iliyookotwa 6g
(ii) Tende kilo 1800
(iii) Mbuzi na kondoo 80
(iv) Thamani ya mali ya biashara Tsh
400,000/=
(v) Fedha taslimu Tsh 200,000/=
(vi) Cheni ya fedha (silver) iliyookotwa 5g
A. Mbuzi 2 au kondoo 2 au mbuzi 1
na kondoo 1
B. 0.5g
C. Tsh. 10,000/=
D. Kilo 180
E. 1.2g
F. 0.75g
G. Mbuzi 2 au kondoo 2
H. Tsh 5,000/=
SEHEMU B (Alama 54)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Miongoni mwa mambo ya ghaibu ni kuamini Malaika wa Allah.
(a) Toa sababu moja madhubuti kwanini hawaonekani kwa wanadamu?
(b) Bainisha kwa hoja moja kwa namna gani mwanadamu anaweza kuwa bora ili hali
Malaika hawamuasi Allah kabisa?
4. Umepewa fursa ya kuishauri serikali yako juu ya masuala ya usalama wa nchi. Kwa kurejea
historia ya Uislamu Madinah wakati wa Mtume (Sallallahu Alayhi Wasallam) tumia hoja tatu
kuonesha namna utakavyoishauri.
5. Umejiwa na Muislamu aliyezini ili hali hajaoa, mwingine amemkata mwenzie kidole na
mwingine amemtukana ndugu yake. Wafahamishe kwa ufupi aina za makosa yao na hukumu
zake ili wasije kurejea tena wakaangamia.
6. Kirobo ni mwanamke aliyejaaliwa kupata watoto wanne kwa mume wake wa ndoa, na hataki
tena kupata mtoto kwa sababu ni kinyume na alivyoshauriwa alipokwenda zanahati, japo
mumewe hataki. Kwa kuzingatia Uislamu tumia hoja tatu kutatua mzozo huu.
7. Katika jamii yako kuna matendo mengi yanafanywa yanayokwenda kinyume na haki na
uadilifu na watu hao wanadai kuwa ni vigumu kuishi kwa kutenda haki kutokana na
mazingira. Tumia hoja tatu kuwaonesha kuwa inawezekana jamii hiyo kuondokana na hali
hiyo mbaya.
8. Wanafunzi wa kidato cha tatu wanatamani kujua historia ya Maswahaba baada ya kutawafu
Mtume (Sallallahu Alayhi Wasallam) hasa katika kipengele cha kuporomoka kwa Dola ya
Kiislamu. Tumia hoja tatu kuwafahamisha sababu zilizopelekea jambo hili baya kutokea.
Page 5 of 5
SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili tu katika sehemu hii
9. Ndugu yako ni tajiri sana lakini hatoi zakat kwa kudhani kuwa atafirisika. Mshawishi ndugu
huyu kwa kumueleza faida nne zinazotokana na utekelezaji wa ibada hiyo.
10. Umekutana na asiye Muislamu na anaichukia Qur’an kwa kudai kuwa si kitabu cha Allah bali
ni maneno ya Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam). Dhaifisha dai lake hili kwa
kumpa hoja tano madhubuti kutoka kwenye Qur’an yenyewe.
11. Darasani kwenu kuna mwanafunzi analingania watu kwa kutumia matin ya Hadith isiyo
sahihi kwa kuwa hajui fani ya Hadith za Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam)
hasa kwenye kipengele cha matin. Muelimishe ndugu huyo sifa tano za kipengele hicho
zinazokifanya kiwe sahihi. Wabillah Tawfiiq
No comments:
Post a Comment