Wednesday, September 4, 2024

ZOEZI NA 2

2.            Orodhesha tofauti sita baina ya malaika na wanadamu.

3.            (a) Kwa kutumia hoja tatu, bainisha udhaifu wa madai kuwa Mahari inashusha hadhi ya mwanamke.

(b)  Toa sabdbu tatu za mwanamke wa Kiislamu aliyefiwa na mumewe kukaa Eda.

4.            (a) Tathmini faida tatu walizopata Waislamu baada ya matokeo ya vita ya Badr.

(b)  Linganisha vitimbi vitatu vya wanafiki wa Madina walivyomfanyia Mtume Muhammad (S .A.W) na vile wanavyofanyiwa Waislamu wa leo.

5.            (a) Bainisha lengo la kuumbwa kwa mwanadamu.

(b)  Kwa kutumia hoja mbili, onesha tofauti kati ya mwanadamu na mnyama.

6.            Tumia hoja mbili kufafanua mgawanyo wa haki za Mwenyezi Mungu (S.W) kwa mujibu wa uislamu.

7.            Chambua ishara tatu zilizowaongoza Waislamu kumchagua Abubakar (R.A) kuwa Khalifa wa kwanza baada ya kutawafu Mtume (S.AW).

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) katika sehemu hii.

8.            Bainisha changamoto nne zinazosababisha kutoonekana kwa matokeo ya ibada ya Hijja.

IO. Fafanua vigezo vinne vinavyotumika kubaini tofauti kati ya sura za Quran zilizoteremshwa Madinah?

11. Miongoni mwa upotofu wa wazi katika Dini ya Uislamu ni kukataa nafasi ya Hadithi za Mtume (S.A.W) kama msingi mkuu wa shei•ia. Bainisha udhaifu wa hoja tatu za wapinzani wa msingi huo. 

EDK SERIES NA 1

 Page 1 of 5

BARAZA LA WAKUU WA SHULE ZA KIISLAMU TANZANIA

MTIHANI WA UTAMILIFU WA SHULE ZA KIISLAMU KIDATO IV

ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

(Kwa Watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

MUDA: SAA 3 Ijumaa, 25 Agosti 2023 mchana

Maelekezo

1. Mtihani huu una sehemu tatu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).

2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C.

3. Hakikisha unasoma maelekezo ya kila swali kwa umakini.

4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

5. Hakikisha unaandika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha

kujibia.

015

Page 2 of 5

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo

kwenye kijitabu chako cha kujibia.

(i) Umewakuta wanafunzi wa kidato cha kwanza wakibishana juu ya nafasi ya elimu

katika Uislamu. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo inaonesha usahihi wa jambo

wanalobishana?

A. Elimu ndio amri ya kwanza kwa mwanadamu

B. Elimu ya mazingira ndio amri ya kwanza kwa mwanadamu

C. Elimu ya akhera ndio amri ya kwanza kwa mwanadamu

D. Elimu ya swala ndio amri ya kwanza kwa mwanadamu

E. Elimu ya dunia na Akhera ndio nyenzo ya kuwa na maisha mazuri

(ii) Ifahamishe jamii yako kosa walilofanya watu wa Madyan ili wasipate ghadhabu za

Allah duniani na Akhera kati ya haya yafuatayo:

A. Kuchanganya haki na batili

B. Kuabudu masanamu

C. Kujifakharisha

D. Kupunja vipimo

E. Kuua Manabii wa Allah

(iii) Umeombwa usimamie mazishi ya jirani yako Muislamu. Jambo gani utawaongoza

watu kufanya mara tu baada ya kuzika?

A. Kusoma Yaa Siin juu ya kaburi

B. Kulipa madeni ya maiti

C. Kumlakinisha maiti

D. Kumuombea msamaha maiti

E. Kudhikiri kwa adhkar

(iv) Mdogo wako anafanya ibada maalumu huku akicheza kamari, hii ni kwa sababu hajui

uhusiano uliopo kati ya ibada hizo na lengo la maisha yake. Maelezo yapi kati ya

yafuatayo yanaonesha uhusiano huo?

A. Kutekeleza wajibu wa maisha

B. Kujiepusha na moto wa Allah

C. Kufikia lengo la kuumbwa

D. Kufikia hadhi ya Ukhalifa

E. Kupata pepo ya Allah

(v) Ikitokea ndugu yako amekasirika kiasi cha kutaka kumdhuru rafiki yake, utamshauri

afanye nini ili kudhibiti hali hiyo?

A. Amswalie Mtume

B. Alete Takbir

C. Alete Istiadha

D. Alete Bismallah

E. Alete Tahlil

Page 3 of 5

(vi) Mtaani kwenu kumezuka hofu kubwa ya watu kusumbuliwa na wachawi. Utaishauri

nini familia yako kufanya?

A. Kuchoma udi rohani

B. Kuchoma ubani Maka

C. Kusoma muawidhatain

D. Kuweka zindiko mlangoni

E. Kutundika Yaa Siin mlangoni

(vii) Vipengele vipi kati ya vifuatavyo utavitumia kumfahamisha ndugu yako sehemu za

Hadith katika uandishi wake ili aitambue Hadith kamili?

A. Isnad, Matin na Riwaya

B. Matini Rawi na Isnad

C. Riwaya, Rawi na Sanad

D. Sanad, Isnad na Matin

E. Rawahu, Riwaya na Rawi

(viii) Umempa kazi mwanafunzi mwenzio akubainishie sifa za mpokezi wa Hadith

akaorodhesha sifa tano. Sifa hizi zote ni sahihi ISIPOKUWA ipi?

A. Ukweli

B. Uadilifu

C. Udhibitifu

D. Ucha Mungu

E. Umri

(ix) Mzee Tondo anajitahidi kuhudumia familia yake vizuri kwa kuwalisha vizuri,

kuwavisha vizuri, kwa sababu ana kazi inayompatia kipato kizuri. Mzee huyu

ameepukana na Dini gani?

A. Utawa

B. Ukafiri

C. Ushirikina

D. Dini za watu

E. Dini ya Shetani

(x) Bwana Manyasi ni mpiga ramli maarufu. Bwana huyu anakwenda kinyume na Taw-

hid gani?

A. Malezi ya Allah

B. Majina na sifa za Allah

C. Ibada maalumu za Allah

D. Hukumu na sharia za Allah

E. Mamlaka ya Allah.

Page 4 of 5

2. Oanisha mali zinazojuzu kutolewa zakat zilizokidhi vigezo vyote zilizo katika Orodha A na

viwango vinavyostahiki kutolewa vilivyo katika Orodha B kisha jaza herufi ya jibu sahihi

katika kijitabu chako cha kujibia.

ORODHA A ORODHA B

(i) Dhahabu iliyookotwa 6g

(ii) Tende kilo 1800

(iii) Mbuzi na kondoo 80

(iv) Thamani ya mali ya biashara Tsh

400,000/=

(v) Fedha taslimu Tsh 200,000/=

(vi) Cheni ya fedha (silver) iliyookotwa 5g

A. Mbuzi 2 au kondoo 2 au mbuzi 1

na kondoo 1

B. 0.5g

C. Tsh. 10,000/=

D. Kilo 180

E. 1.2g

F. 0.75g

G. Mbuzi 2 au kondoo 2

H. Tsh 5,000/=

SEHEMU B (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Miongoni mwa mambo ya ghaibu ni kuamini Malaika wa Allah.

(a) Toa sababu moja madhubuti kwanini hawaonekani kwa wanadamu?

(b) Bainisha kwa hoja moja kwa namna gani mwanadamu anaweza kuwa bora ili hali

Malaika hawamuasi Allah kabisa?

4. Umepewa fursa ya kuishauri serikali yako juu ya masuala ya usalama wa nchi. Kwa kurejea

historia ya Uislamu Madinah wakati wa Mtume (Sallallahu Alayhi Wasallam) tumia hoja tatu

kuonesha namna utakavyoishauri.

5. Umejiwa na Muislamu aliyezini ili hali hajaoa, mwingine amemkata mwenzie kidole na

mwingine amemtukana ndugu yake. Wafahamishe kwa ufupi aina za makosa yao na hukumu

zake ili wasije kurejea tena wakaangamia.

6. Kirobo ni mwanamke aliyejaaliwa kupata watoto wanne kwa mume wake wa ndoa, na hataki

tena kupata mtoto kwa sababu ni kinyume na alivyoshauriwa alipokwenda zanahati, japo

mumewe hataki. Kwa kuzingatia Uislamu tumia hoja tatu kutatua mzozo huu.

7. Katika jamii yako kuna matendo mengi yanafanywa yanayokwenda kinyume na haki na

uadilifu na watu hao wanadai kuwa ni vigumu kuishi kwa kutenda haki kutokana na

mazingira. Tumia hoja tatu kuwaonesha kuwa inawezekana jamii hiyo kuondokana na hali

hiyo mbaya.

8. Wanafunzi wa kidato cha tatu wanatamani kujua historia ya Maswahaba baada ya kutawafu

Mtume (Sallallahu Alayhi Wasallam) hasa katika kipengele cha kuporomoka kwa Dola ya

Kiislamu. Tumia hoja tatu kuwafahamisha sababu zilizopelekea jambo hili baya kutokea.

Page 5 of 5

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili tu katika sehemu hii

9. Ndugu yako ni tajiri sana lakini hatoi zakat kwa kudhani kuwa atafirisika. Mshawishi ndugu

huyu kwa kumueleza faida nne zinazotokana na utekelezaji wa ibada hiyo.

10. Umekutana na asiye Muislamu na anaichukia Qur’an kwa kudai kuwa si kitabu cha Allah bali

ni maneno ya Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam). Dhaifisha dai lake hili kwa

kumpa hoja tano madhubuti kutoka kwenye Qur’an yenyewe.

11. Darasani kwenu kuna mwanafunzi analingania watu kwa kutumia matin ya Hadith isiyo

sahihi kwa kuwa hajui fani ya Hadith za Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam)

hasa kwenye kipengele cha matin. Muelimishe ndugu huyo sifa tano za kipengele hicho

zinazokifanya kiwe sahihi. Wabillah Tawfiiq