Tuesday, February 23, 2016

Kuongeza Msamiati Wa Kiswahili

Uundaji wa Maneno
Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe.
Njia za Uundaji Maneno
Elezea njia mbalimbali za uundaji maneno
Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:
  1. Kubadili mpangilio wa herufi.
  2. Kuambatanisha maneno.
  3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine.
  4. Uambishaji wa maneno.
  5. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura.
Kuunda msamiati kwa kubadili mpangilio wa herufi
Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine
Example 1
Mfano
  • Neno lima, lina herufi l, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali, kumi,imla, mila.
  • Neno tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:- tatu, tua, viatu, tatua.
Njia ya kuambatanisha maneno
Kuna njia tatu za kuambatanisha meneno
Njia ya kurudufisha au kukariri neno
Mfano; barabara, sawasawa, polepole, katikati, vilevile.
Njia ya uundaji wa Msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofauti
Nomino na Nomino
  • Punda + mlia unapata Pundamilia
  • Bibi + Shamba unapata Bibishamba
  • Afisa + Elimu unapata Afisaelimu
  • Mwana + Siasa unapata Mwanasiasa
  • Bata + maji unapata Batamaji
Kuunganisha kitenzi na Nomino/Jina
  • Changa + moto changamoto
  • Chemsha + bongo chemshabongo
  • Piga + mbizi pigambizi
  • Zima + moto zimamoto
Kuunganisha maneno mawili na kudondosha baadhi ya herufi
Example 2
Mfano
  • Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA
  • Mzaliwa wa mahali Fulani MZAWA
  • Chama cha Mapinduzi CCM
  • Nyamamfu NYAMAFU
Kutohoa maneno kutoka lugha nyingine
Kila lugha na tabia ya kuchukua maneno lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya Msamiati. Maneno kutoka lugha nyingine yanapoteuliwa hubadilishwa kimatamshiili ya fuate kanuniza Kiswahili.
Maneno yanayotoholewa kutoka lugha nyingine husanifishwa na asasi za lugha ya Kiswahili ndipo ya ruhusiwe kutumiwa rasmi.
Example 3
Mfano
Neno la KiswahiliLugha ya MwanzoNeno Lililotoholewa

Kijerumani Schule
Salama Kiarabu Salaam
Duka KihindiDukan
KarotiKiingerezaCarrot
ShatiKiingerezaShirt
PichaKiingerezaPicture
PapaiKihispaniaPapaya
MezaKirenoMezi
ShukraniKiarabuShukran
NgeliKihayaEngeli
IkuluKinyamweziIkulu
Ng'atukaKizanakiNg'atuka
NdafuKichagaNdafu
Namba

Kuunda maneno kwa njia ya uambishaji wa maneno
Hii ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwe nyekiini. Ujenzi wa maneno hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana zina husiana.
Mfano mzizi: -lim-.Tukipachika viambishi awali na tamati tunapata maneno kama lima, analima, walilima, kilimo, limiana,halitalimwa na ukulima.
Kufananisha sauti, sura au tabia
Example 4
Mfano
  • Kengele - utokana na sauti ya kengele inapo pigwa
  • Pikipiki - hutokana na muungurumo wa pikipiki
  • Ndizi mkono wa tembo – Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama tembo
  • Chubwi - Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.

1 comment:

  1. Yaani wewe ni mzalendo ambaye una mfano wa kuigwa. Maana umeamua uwasaidie watanzania wenzako nao wapate kile unachokipata.
    Ni kweli Mungu akubariki sana.

    ReplyDelete